Ticker

6/recent/ticker-posts

WAFUGAJI WAVAMIA HIFADHIU YA TARANGIRE

WAFUGAJI katika Mkoa wa Manyara wanaoishi pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Tarangire wamevamia  hifadhi hiyo na kulisha mifugo yao  kwa kipindi kirefu hasa wakati wa kiangazi na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira.

Maeneo yaliyoathirika kwenye hifadhi hiyo ni eneo la vijiji vya

GijedabongWaloa,Basoda,Ayamango,Gedamar,Mamire,Eshkesh,Chubi,Kimotorok,Mswakini
 Juu,Endakiso na Mswakini chini.

Akizungumza mjini Babati  na wenyeviti na maofisa watendaji wa vijiji vinaozunguka hifadhi hiyo,Kaimu Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya Tarangire,Dk James Wakibara alisema vijiji vya Loiborsiret na Lobosoit uingizaji wao ni mdogo.


Dk Wakibara alisema madhara yanayotokana na uingizaji wa mifugo hifadhini ni kuenea kwa magonjwa ya maambukizi kutoka kwa wanyama wafugwao kwenda kwa wanyama pori na mmomonyoko wa udongo.


Alitaja sababu za kuingiza mifugo hifadhini ni uhaba wa maeneo ya malisho, kuongezeka kwa mashamba makubwa kwa ajili ya kilimo,ufugaji wa mifugo mingi usiozingatia ushauri wa kitaalamu,ukame unaotokana na uhaba wa mvua na ongezeko la idadi ya watu katika maeneo yanayopakana na hifadhi.


Kwa upande wake,Mhifadhi ujirani mwema wa hifadhi ya Tarangire,Lomi Ole Meikasi alisema sehemu ya maendeleo ya Tanzania inategemea kwa kiasi kikubwa wanyama pori na utajiri ulio katika mifumo ya ikolojia anuai.


Ole Meikasi alisema shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) ilianzisha mwaka 1959 na hifadhi ya Tarangire iliyopo kaskazini mwa nchi ilianzishwa mwaka 1970 na inaukubwa wa kilomita za mraba 2850.


Alisema ikolojia ya hifadhi ya Tarangire imegawanyika kwenye misimu miwili ya kiangazi na masika ambapo kipindi cha masika makundi ya wanyama kama nyumbu,pundamilia,twiga,tembo na nyati hutoka hifadhini na kuelekea mbuga ya Simanjiro.


Alisema hifadhi ya madhumuni makubwa ya hifadhi za Taifa ni kuhifadhi maeneo yaliyo na thamani au sifa ya kipekee zinazoonyesha urithi wa mali za kitamaduni au maliasili za Tanzania.

Post a Comment

0 Comments