WANANCHI WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUCHANGIA KATIBA NA SENSA
Serekali wilayani hai imetoa wito kwa wananchi wa wilaya hiyo
kujitokeza kwa wingi wakati wa mchakato wa mjadala wa katiba pindi
tume iliyoteuliwa na rais Jakaya mrisho Kikwete itakapofika wilayani
humo
Hayo yalibainishwa na mkuu wa wilaya ya hai Novatus makunga wakati alipokuwa akiongea na polisi ili kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili.
Akizungumza na polisi hao alisema kuwa kila mtanzania anayo haki ya kushiriki mjadala wa katiba na kutoa maoni yake wakati ukifika akiwemo polisi pamoja na wananchi wengine .
mkuu huyo wa wilaya alisisitiza kuwa katiba ya nchi siyo ya mtu mmoja ama kiongozi mmoja ama chama chochote cha siasa bali ni katiba ya watanzania wote kwa manufaa yao wote bila kujali itikadi za vyama vyoa vya siasa.
Aidha alisema kuwa kutokaana na hayo kila mwananchi ambaye ni mtanzania anawajibu wa kushiriki katika mjadala huo na ni fursa pekee ambayo rais ameitoa kwa watanzania .
Makunga akizungumzia swala la sensa ya watu na makazi aliwataaka wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza wote katika makazi yao ili waweze kuhesabiwa hapo ifikapo mwezi Agosti 26 mwaka huu huku akitoa wito kwa wannachi kutoa taarifa zote muhimu na sahii kutokana na maswali yaliyopo katika madodoso ya sensa.
Alibainisha kuwa sensa ya watu na makazi inaiwezesha kuandaa mipango ya maendeleo kwa uakini na usahii na kwa ubora zaidi katika kuleta maendeleo na tija kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Aidha alibainisha kuwa sensa ya makazi na watu inawezesha serekali kutoa huduma kwa kwa wananchi wake zilizobora kutokana na kuwa na uhakikia na twakwimu za watu wake juu ya mipango endelevu huku akitoa onyo kwa wananchi kuepuka kuwaficha watu wenye ulemavu wa aina yeyote kwani kundi hilo pia lina haki ya kuhudumiwa na serekali kama mwananchi mungine yeyote yule.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia