WANAKIJIJI WAFUNGA OFISI YA KIJIJI KWA KUWATUHUMU MWENYEKITI NA OFISA MTENDAJI KWA UBADILIFU

WAKAZI wa Kijiji cha Luxmanda Wilaya ya Babati Mkoani Manyara
wamefunga na kufuli ofisini ya kijiji hicho hivyo kuwazuia Mwenyekiti
na Ofisa mtendaji wa kijiji hicho kwa madai ya tuhuma mbalimbali
ikiwemo ubadhirifu.

Wakizungumza na libeneke la kaskazini kijijini hapo wananchi hao
walidai kuwa viongozi hao wamekuwa wanakiongoza kijiji hicho bila
kufuata utaratibu ikiwemo kutowasomea mapato na matumizi kwa zaidi ya
miaka minne.

Walisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakikiendesha kijiji hicho kama
wanavyotaka wenyewe kwani wanafanya maamuzi bila kuwashirikisha
wanakijiji hao ikiwemo kutotambuwa hatma ya fedha za kijiji chao.

“Waende wakaongoze sehemu nyingine siyo hapa kwetu sisi ndiyo
tumewaajiri lakini imekuwa tofauti kabisa sasa kilichobaki ni wao
wakapewe ofisini kule kwa mkurugenzi wa halmashauri kwani imekuwa
kero,” walisema wananchi hao.

Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Babati vijijini,Chediel Mrutu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo la
viongozi wa kijiji hicho kuzuiliwa kuingia ofisini kwao.

Hata hivyo,Mrutu alisema wananchi hao wamefanya makosa kwa kuwazuia
viongozi wao kuingia ofisini kwani kama kulikuwa kuna makosa
wangechukua hatua nyingine za kisheria zinazotakiwa na siyo kufunga
ofisi.

Alisema anatarajia kukutana na wananchi wa kijiji hicho ili
kuwaelewesha na kuwapa utaratibu wa kuchukua endapo wanaona kuwa
viongozi wa kijiji hicho kuna mahali wamekosea katika utendaji kazi
wao.

Matukio ya wakazi wa wilaya ya Babati kufunga ofisi za vijiji yamekuwa
yakitokea mara kwa mara ambapo mwishoni mwa mwezi uliopita wakazi wa
kijiji cha Endaw waliifunga ofisi ya mtendaji kwa kudai kushindwa
kuwajibika.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia