SPIKA WA TATU WA BUNGE LA EALA NI MWANA MAMA

Spika wa tatu wa Bunge jipya la Afrika Mashariki (EALA) Margaret Banbtonbg
Zziwa (49) kutoka Uganda akitoka ndani ya Ukumbi wa Bunge hilo uliopo
katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC jijini Arusha leo. Zziwa ambaye ni Mchumi
kitaaluma amemshinda mwanamke mwingine kutoka Uganda, Mwanasheria Dora
Byamukama (40) baada ya uchaguzi huo kurudiwa mara mbili baada ya kura za
awali kutokufikia idadi asiliamia 30 inayotakiwa ya wapiga kura wote



WABUNGE wa bunge la Afrika mashariki wamemchagua spika wa bunge hilo kutoka nchini Uganda ambaye ataliongoza bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Spika huyo ambaye ndio mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo wa juu katika bunge hilo ni Magreth Zziwa kutoka nchini Uganda mbaye alimbwaga mpizani wake Dora Byamukama ambaye naye anatoka nchini Uganda.

Katika kura za awali matokeo ya kura hayakumpa Zziwa nafasi hiyo baada ya kupata kura 27 huku mpinzani wake kura 18 na kufanya uchaguzi huo kurudiwa upya.

Mwanamama huyo atakeyeliongoza bunge hilo kuanzia sasa ni msomi mchumi mwenye shahada ya uzamili wa sayansi ya siasa na uchumi.

Baada ya zoezi hilo kurudiwa Spika huyo aliibuka tena kwa ushindi mnono wa kura 33 dhidi ya 12 za mpinzani wake.

Mara baada kuchaguliwa Spika huyo aliapishwa kwa mujibu wa taratibu za bunge hilo ambapo baada ya kula kiapo aliwashukuru wabunge wa bunge hilo kwa kumchagua.

“Naishukuru serikali yangu ya Uganda na pia wananchi wa Uganda na ninyi wabunge kwa kunichagua kushika wadhifa huu nawaomba ushirikiano tuendleze jumuiya yetu”alisema Zziwa.

Mara baada ya zoezi hilo wabunge 45 wa jumuiya waliapishwa rasmi kuwa wabunge wa bunge hilo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Uchaguzi huo wa spika wa bunge hilo ulihudhuriwa na watu mbalimbali kutoka nchi za afrawali badhin ya ndugu waliokuwa wakifuatilia uchaguzi huo kwa njia ya luninga zilizofungwa nje ya ukumbi wa bunge hilo walipongeza namna uchaguzi huo ulivyoendeshwa.
Bunge hilo ambalo linazinduliwa kwa mara ya tatu na kuongozwa na Maspika kutoka nchi wanachama ambao huchaguliwa kwa kupokezana lilianza mwaka 2001 ambapo liliongozwa na SSpika kutoka Tanzani Abdulrahaman Kinana kabla ya kupokelewa na Mkenya anayemaliza muda wake Abdrahin Abdi.

Kazi kubwa ya bunge la afrika Mashariki ni kusimamia na kutunga sheria mbalimbali za uendeshaji wa mambo katika jumuiya hiyo iliyo mbioni kuwa shirikisho la Afrika mashariki.





About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia