WADAU WA SEKTA YA UTALII WAPANDA MITI 1000

WADAU wa sekta ya Utalii mkoa wa Arusha, kupitia Chama cha waongoza watalii, nchini TATO,leo wamepanda miche ya miti zaidi ya 1000, aina mbalimbali ikiwa ni katika kuadhimisha wiki ya bonanza la  Utalii mkoani Arusha linaloshirikisha waongoza utalii na wamiliki wa Hotel ..

Mratibu wa shughuli hiyo, Armstrong Nyaka, amesema kuwa miti hiyo imepandwa katika bonde la mto Themi mjini Arusha na lengo lao ni kupanda miti 2000 ambapo iliyobakia itapandwa siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya Utalii June 5 mwaka huu.

Amesema kuwa maadhimisho hayo yaitwayo, Karibu faire ,yanalenga kuwakutanisha wadau wa usafiri kuboresha afya zao sanjari na kutunza mazingira ili waelewe umuhimu wa kuishi kwenye mazingira mazuri na safi ambayo yanapendeza hata wakati wanapoongoza watalii basi maeneo yote yawe ni kijani.

hivyo akatoa wito kwa wadau wa mazingira mjini Arusha,kujitokeza kwa wingi siku ya kilele ambayo itakuwa Juni 5 mwaka huu ili waweze kushiriki kupanda miti katika maeneo mbalimbali ya jiji la arusha.

Ameongeza kuwa kila mwaka wadau wa utalii mkoani Arusha huwa wanaadhimisha bonanza la utalii kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na michezo ya mpira wa miguu, kurusha mikuki, kuvuta kamba, kuruka na magunia ambapo timu zinazoshinda huwa zinapewa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha na vikombe .

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia