Ticker

6/recent/ticker-posts

 Rais mstaafu Benjamini mkapa akisoma hutuba yake katika mkutano wa ICF
waandishi wa habari  wakijadili jambo mara baada ya kutoka kwenye mkutano wa ICF
 
 
Mtendaji Mkuu wa ICF, Omary Issa amesema  kuwa ICF imesaidia  kuboresha mfumo wa usajili wa makampuni nchini Rwanda ambapo kwa sasa humchukua mtu siku 2 kusajili biashara tofauti na awali ambapo ilikuwa wakitumia mpaka siku 16 huku gharama zikipungua kutoka dola za Marekani 433 mpaka 25.
 
Issa alisema kuwa taasisi yake katika kuhakikisha shughuli za biashara zinafanyika kwa urahisi na ufanisi zaidi imesaidia kuboresha mfumo wa mahakama nchini Zambia kwenye mahakama 3 na kutoa mafunzo kwa majaji wapya 14 huku nchini Sierra Leone wakifanikiwa kuboresha mfumo wa mahakama ambapo kwa sasa huchukua miezi miwili tokea kufungua kesi za biashara na kupata uamuzi ambapo awali ilikuwa inatumia mpaka miaka sita 

 alisema kuwa taasisi hiyo inashirikiana na  TRA na Jeshi la polisi nchini kuboresha utoaji huduma kwa kuhakikisha bidhaa zinazopita nchini (transit goods) kwenda nchi jirani ya Rwanda zinasafirishwa kwa usalama na haraka kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Rusumo kwenye mpaka wa nchi hizo hivyo kupunguza gharama za usafirishaji.
 
Hayo yalisemwa na afisa wa TRA, Alexander Buchafwe, alipokuwa akitoa maelezo kwenye  banda ya taasisi za serikali za nchi za Afrika zilizonufaika na Taasisi ya kuboresha uwekezaji Afrika (ICF) ambayo inafanya  mkutano wake  pili mkubwa wa  kimataifa kwenye hoteli ya Naura Spring.
  
Alisema kuwa mfumo huo ulizinduliwa rasmi Machi 12, mwaka huu ambapo wamewapa wamiliki wote wa magari ya mizigo muda wa miezi mitatu wawe wamefunga vifaa hivyo kutoka kwa  makampuni sita waliothibitishwa na TRA kwa ajili ya kufanya kazi ya kuuza na kufunga vifaa hivyo.

Post a Comment

0 Comments