BARAZA la mkoa la Chama cha
Walimu, CWT, limewataka walimu kote nchini kushiriki kwenye mgomo wan chi nzima
ambao utaanza Julai, 7 mwaka huu , ikiwa ni shinikizo la madai ya nyongeza ya
mishahara na posho za kujikimu na kufanya kazi kwenye mazingira magumu, na
kuwata wazazi kuwaunga mkono katika mgomo huo.
Taarifa iliyotolewa mara baada
ya kikao cha siku moja cha kujadili hatua za kuchukua kilichofanyika katika
ofisi ya Chama cha Walimu ,CWT, mkoa wa Arusha, imesema kuwa baraza limeridhia
kuwepo kwa mgomo huo na kuwataka walimu wote kushiriki ikiwa ni shinikizo
la kuitaka serikali kuwatimizia madai yao.
Taarifa hiyo imesama kuwa Walimu
wanadai nyongeza ya mshahara ya 100% ,posho ya kufanya kazi kwenye mazingira
magumu, 55% na30% ni posho ya kujikimu,nyongeza ambayo itawezesha walimu
kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.
Baraza limesema kuwa kutokana na
madai yao kutokushughulikiwa na serikali kwa kipindi kirefu sasa limeamua
kuchukua hatua ya kutangaza mgogoro na serikali hatua ambayo itafuatiwa na
mgomo wa walimu nchini ambao utafanyika mara baada ya walimu kujaza fomu na
kupiga kura za kuunga mgomo Julai 7 mwaka huu.
Baraza limesema kuwa limefuata
taratibu zote za kisheria na kuwatoa hofu walimu k,kuwa hakuna mwalimu atakae
fukuzwa kazi kwa kushiriki mgomo huo kudai maslahi yao na limejipanga
kuhakikisha hakuna mwalimu atakaechukuliwa hatua zozote za kinidhamu katika
kutetea haki yake ya msingi.
Baraza limesema linaunga mkono
maazimio ya Baraza kuu la taifa la CWT, lililofanyika mkoani Dodoma Juni 5
mwaka huu ambapo liliwataka viongozi waCWT, ngazi zote kutekeleza matakwa
ya ya kutangazwa mgogoro kwa mjibu wa sheria za Ajira na mahusiano
kazini,ya mwaka 2004 ,na baraza liliidhinisha kuwepo kwa mgomo ikiwa
serikali itasindwa kutekeleza matakwa ya walimu ya kutaka kuongezewa
mshahara kwa 100%. katika mgomo huo.
Baraza likatoa wito kwa wazazi
nchini kukaa na watoto wao majumbani ili kuepuka kuwapatia usumbufu wakati wa
mgomo wa walimu kwa sababu wakati wa mgomo huo walimu hawatafundisha .
Baraza limesewma kuwamgogoro huo ni
wa kimasilahi ,kwa kuwa serikali haijawa tayari kukaa na Chama cha walimu
nchini kutafuta ufumbuzi wa madai yao wana haki ya kutumia mgomo kama njia ya
kutekelezwa madai yao.
Baraza kuu la taifa ,limesema kuwa
CWT, ilijaza fomu namba 1, ya kutangaza mgogoro na iliwasilishwa kwenye
tume ya Usuluhi na Uamzi, Juni 8 ,mwaka 2012, na mgogoro huo haujatatuliwa hadi
leo licha sheria kutaka mgogoro utatuliwe ndani ya siku 30.
Baraza limesema kuwa Wanaolalamikiwa
kwenye mgogoro huo ni Mkuu wa Utumishi wa Umma, ambae ni Katibu mkuu kiongozi,
Waziri wa Nchiofisi ya rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Katibu mkuu
wizara ya Elimu na mafunzo ya Ufundi,na mwanasheria mkuu wa serikali .
Baraza limesema kuwa fedha zipo na
zimeshatolewa ila zinaliwa na wachache hivyo wanaishinikiza serikali ili
walipwe na limewataka viongozi wa serikali kutokuwatishia walimu kwa kudai
masilahi yao.
Baraza limeongeza kuwa walimu ndio
wafanyakazi wanaodaiwa mikopo mingi kutoka katika taasisi mbalimbali za Umma na
binafsi na hivyo wanaishi katika mazingira magumu ,wanalazimika kuingia kwenye
mikopo kutokana na kulipwa maslahi duni wakati kazi wanzofanya ni kubwa mmno.