WANAFUNZI 36 KULIPIWA ADA

Mfuko wa maendeleo ya Elimu,Kata ya Naisinyai Wilaya ya Simanjiro
Mkoani Manyara,umetenga sh175,000 kwa ajili ya kuwalipia ada na
gharama nyingine wanafunzi 36 wa shule za sekondari wanaoishi kwenye
mazingira magumu.

Akizungumza na libeneke la kaskazini,Diwani wa kata ya
Naisinyai,Klemp Ole Kinoka alisema kwamba wanafunzi watakaofaidika na
mfuko huo ni watoto wanaoishi kwenye kata hiyo pekee na siyo wanafunzi
kutoka nje ya hapo.

Kinoka alisema mfuko huo utawasomesha wanafunzi hao 36 waliopo kidato
cha kwanza na cha pili kwenye shule za sekondari Naisinyai na Ewong’on
zilizopo kwenye kata yake.

Alisema kuwa mfuko wa maendeleo wa elimu wa kata ya Naisinyai
ulianzishwa Juni 28 mwaka 2010 kwa wananchi wa jamii ya wafugaji wa
eneo hilo ambao ndiyo kuchangia mfuko huo kila mwaka.

“Mfuko huo wa maendeleo wa elimu wa kata yangu kwa mwaka jana
uliwasomesha wanafunzi 26 na mwaka huu umewasomesha wanafunzi hao 36
na pia mwakani tunatarajia kusomesha wanafunzi wengine,” alisema
Kinoka.

Alisema mfuko huo ambao ni endelevu umelenga kumkomboa mwanafunzi wa
jamii ya kifugaji ambao hivi sasa wana mwamko mkubwa wa kupata elimu
kwani wamebaini bila elimu hawawezi kupata maendeleo.

Kata ya Naisinyai ni kata pekee wilayani humo yenye shule mbili za
sekondari ambazo ni Naisinyai na Ewong’on yaani mwanga kwani kata
nyingine zina shule moja moja za sekondari.

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia