WAWEKEZAJI WAKWEPA KODI KUTHIBITIWA
| washiriki wa mafunzo ya semina iliyokuwa imeandaliwa na UNDP | |||||
| SERIKALI imeanzisha
mpango wa kuwadhibiti wawekezaji na wazawa wanaokwepa kulipa kodi na
kulisababishia taifa kukosa mapato ambayo yatasaidia kuboresha huduma
mbalimbakli za jamnii na kukamilisha mira ya maendeleo. Hayo yameelezwa na Naibu mwanasheria mkuu wa Serikali, George Masaju,alipokuwa akifunga mafunzo ya siku tano taliyofadhiliwa na shirika la mipango na maendeleo la Umioja wa mataifa UNDP, kwa wataalamu kutoka wizara mbali mbali za Tanzania bara na Zanzibar, kuhusu mianya inayotumiwa na wawekezaji kukwepa kulipa kodi . Masaju, amesema kutokana na kuwepo mianya hiyo ambayo inasababisha ukwepaji serikali imeaanzisha mafunzo hayo kwa wataalamu kutoka wizara mbalimbali ili kudhibiti hasa kwenye miradi mikubwa ya madini ikiwemo mafuta ya Petrol, na Gesi ambako kuna onekana kuna mianya mingi ya ukwepaji wa kodi unaofanywa na baadhi ya wawekezaji wasikuwa waaminifu. Amesema ukwepaji mkubwa hujitokeza kwa wawekezaji katika kipindi cha mpito ambapo huwa wanabadili majina kabla ya muda wa mpito kwisha ili kukwepa kulipa kodi hivyo kuanzia sasa serikali imejidhatiti kikamilifu kudhibiti ukwepaji huo. Amesema serikali imeaanzisha mpango kabambe wa kusomesha wataalamu wake ili kuondokana na mikata mibovu ambayo imekuwa ikitusababishia matatizo na hasara kubwa kwa sababu inatoa mianya na hivyo kulikoseha taifa mapato yanayotokana na raslimali zake. Amesema kuna wawekezaji wa aina mbili wapo ambao hufuata taratibu na hao huwa wanalipa kodi zao bila matatizo ,ila kundi la pili la wawekezaji wasiokuwa waaminifu huwa wanatumia ujanja kukwepa kulipa kodi na kusababisha taifa kukosa mapato ambayo yanegelisaidia kuondoa umasikini ambalo ni tatizo kubwa nchini. Amesisitiza kuwa ulipaji kodi ni muhimu kwa ajili ya kuinua uchumi hivyo akawataka wawekezaji kila mmoja kuhakikisha analipa kodi ili kuwezesha taifa kusonga mbele katika kutekeleza miradi mbalimbali ambayo itasaidia kuondoa umaskini kwa wananchi |
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia