Ni wajibu wangu kutamka rasmi kwamba mahakama za gacaca sasa zimefungwa,’’ Rais waRwanda, Paul Kagame alisema mbele ya Bunge mjini Kigali Jumatatu.
Mahakama za gacaca
zilianzishwa nchiniRwanda kushughulikia maelfu ya washitakiwa wa mauaji
ya kimbari ya mwaka 1994, ambapo katika hali ya kawaida zisingeweza
kushughulikiwa kikamilifu na mahakama za kawaida kutokana na uwingi wa
kesi hizo.
‘’Mahakama za gacaca
zimedhihirisha uwezo waRwandawa kuweza kujitafutia suluhisho wenyewe kwa
matatizoyaona watu wake kufanya maamuzi juu ya mambo yanayohusu
maishayao,’’ Rais aliongeza.
Alisisitiza kwamba ‘’haki katika
mahakama za gacaca ilisimamiwa vilivyo na kwa niaba ya watu wenyewe,’’
na kuhitimisha kwamba matokeo ya mwenendo mzima ‘’umezidi matarajio
yetu.’’
Mahakama za gacaca zimetoa hukumu zaidi ya milioni mbili tangu kuanzishwa kwake Juni 2002.
Kwa mujibu wa Rais Kagame,kufungwa
kwa mahakama za gacaca haina maana kwamba ‘’watuhumiwa waliobaki wa
mauaji ya kimbari’’ hawataadhibiwa iwapo watakamatwa. Alisema utaratibu
wa kisheria umewekwa kwa ajili ya watu wa aina hiyo.