WATAKIWA KUTAFUTA UFUMBUZI WA KUZUIA WAKWEPA KODI
WAKUU wa idara mbalimbali za serikali kote nchini wameshauriwa kutafuta ufumbuzi wa namna ya kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi unaoisumbua serikali kwa muda mrefu.
Hayo
yalisemwa naibu waziri wa sheria na katiba Angela Kairuki wakati akifungua
mafunzo ya siku tano ya kujadili kuhusiana na ukusanyaji ya kodi kupitia
mikata mbalimbali katika sekta za nishati ,madini na mafuta ambayo inaendelea jijini hapa.
Alisema
kwa muda mrefu Tanzania na hata nchi zingine za afrika mashariki na frika kwa
ujumla imekuwa ikisumbuliwa na tatizo la ukwepaji kodi kutoka kwa makampuni
makubwa ya uchimbaji wa madini na mafuta kupitia nyanja mbalimbali.
Kairuki
alizitaja nyanja hizo zinazohusika na ukwepaji wa kosi hizo kuwa ni kupitia
uhamisho wa makampuni hayo kwa kudai kuwa kampuni moja iliyopo Tanzania
na tawi jingine nchi za nje kukwepa kulipa kodi kwa madai kuwa ilishalipa
nchini humo.
“mafunzo
haya pia yataisaidi kuwaongezea uwezo zaidi wataalamu hawa ambao wapo katika
mafunzo haya na ninaimani kabisa tukitoka hapa kila mmoja ataendafanya kazi kama vile alivyopata mafunzo
Alisema
kufanikiwa kupatikana kwa majibu ya namna ya kudhibiti mianya hiyo ya kodi
kutawezesha nchi kunufaika na kodi hizo katika kuboresha sekta mbalimbali
zikiwemo za elimu,maji,afya,miundo mbinu na nyingine nyingi.
Alisema
uwezekano wa kupatikana kwa majibu hayo ni mkubwa kutokana na semina hiyo
kuendeshwa na watu kutoka nchi zilizofanikiwa katika kupambana na tatizo hilo ambayo ni Marekani.
Sekta
zinazoshiriki katika mafunzo hayo ni pamoja na mamlaka ya mapato
Tanzania(TRA),Kituo cha uwekezaji cha taifa(TIC),Shirika la uagizaji wa mafuta(TPDC),Shirika
la mazingira la taifa(MEM),Shirika la uchukuzi(MOT)Wizara ya fedha(MOF),Ofisi
ya mwanasheria mkuu wa serikali bara na Zanzibar(AGC)Ofisi ya waziri mkuu(PMO)
na Wizara ya mambo ya nje.
Semina
hiyo ya siku tano ambayo ni ya tisa kufanyika hapa nchini inayoendelea mkoani
hapa imeandaliwa na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali chini ya ufadhili wa
shirika la UNDP inayoongozwa na wakufunzi Stephen Shay na Edward Osterberg wote
kutoka chuo kikuu cha Harvard cha nchini Marekani.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia