AUWSA YABAINI KUHUJUMIWA NA BAADHI YA VIGOGO NA WAFANYAKAZI
MAMLAKA ya maji safi na
maji taka jijini Arusha(AUWSA )imebaini kuhujumiwa wa watu mbalimbali wakishirikiana
na wafanyakazi wake wasio waaminifu kwa kuunganisha maji kinyume cha utaratibu
na kufanya kuwepo kwa upotevu mkubwa wa
mapato.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa
AUWSA,Eng.Ruth Koya amesema kuwa tayari wamefanikiwa kuwanasa wezi wa maji zaidi ya 100 waliojiunganishia kinyume
na utaratibu wakiwemo vigogo wa halimashauri ya Arusha vijijini,ambao wamekuwa
wakitumia huduma hiyo kwa kipindi kirefu
bila kulipa chochote na kuisababishia hasara kubwa kwa mamlaka hiyo.
Vigogo wa halmashauri waliokamatwa
ni pamoja na afisa mali asili, mazingira na ardhi Maico Myairwa ambaye yeye
aling’oa kabisa mita ya idara ya maji ambayo
imekutwa chumbani mwake ameificha huku akijua ni kosa kisheria.
Mwingine ni fundi mkuu wa
maji wa halmashauri ya Arusha,Loishono Mollel ambaye amejiunganishia maji baada ya kutoboa bomba kubwa la idara ya maji
na kupitisha mpira mrefu kwa chini hadi nyumbani kwake ambapo pia alikuwa
akiyatumia maji hayo kustawisha bustani
yake.
Hata hivyo Mollel amebainika
kuwa kinara mwenye mradi wa
kuwaunganishia maji watu mbalimbali kinyemela huku wakimlipa kiasi kikubwa cha
fedha ,ambapo mamlaka hiyo imengóa mtandao wa mabomba yote aliyoyaunganisha kwa wakazi mbalimbali eneo la Seki
na kufanya familia zaidi ya 20 kukumbwa na adha ya kukosa maji.
Pia meneja wa maji wa halmashauri hiyo, Criston Kimaro
ambaye ndiye anadaiwa kutoa idhini ya watu kuunganishiwa maji bila kufuata utaratibu huku
watu hao wakimlipa fedha ya kuwaunganishia pamoja na malipo ya mwezi katika
kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja.
Operesheni hiyo ikiongozwa
na mkurugenzi wa maji safi na maji taka wa jiji la Arusha ,Engineer Koya na kuambatana na maafisa wengine ,imekuja
kufuatia kuwepo taarifa za upotevu mkubwa
wa maji tofauti na kiwango kinachozalishwa kwa siku na kufanya idadi
kubwa ya wateja wake kutopata huduma ya maji safi baada ya nusu ya maji
yanayozalishwa kuishia njiani kwa wajanja wachache.
Eng,Koya alisema kuwa maji
yanayozalishwa na AUWSA ni mengi kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali lakini
amekuwa akishangazwa kupata malalamiko ya kila mara kutoka kwa wateja wake wa kudumu na wapya kwamba hawapati huduma hiyo
.
Alisema kuwa Operesheni
hiyo niyakudumu lengo ni kuhakikisha wanaondoa mtandao wa wezi wa maji ambao
wamekuwa wakijinufaisha bila kuilipa chochote mamlaka hiyo,na kwamba watawafikisha mahakamani watu wote waliohusika
na wizi huo wa maji iwapo watashindwa kulipa fidia katika kiwango walichotumia .
Naye mkuu wa kikosi cha
operesheni wa AUWSA,Mohamed Isumail alisema kuwa tangu kuanza kwa zoezi
hilo,Mei 29 mwaka huu watu zaidi ya 100 kutoka maeneo ya
Moshono,Sekei,Lemara na Ungalimited
wamekamatwa baada ya kubaini
wamejiunganishia huduma ya maji
na kutumia kinyume na utaratibu .
Aidha alisema kuwa maeneo
yaliyokithiri kwa wizi wa maji jijini hapa ni ,Sekei,Moshono Migungani na Baraa
ambapo idadi kubwa ya wakazi wa maeneo hayo wanaiba maji baada ya kuunganisha
mipira mirefu chini ya Ardhi huku wakiwahadhaa waofisa wa maji waporika, kuwa maji
wanayotumia yanatoka kwenye bomba la kijiji ambayo mara nyingi hayalipiwi.
Isumaili ambaye pia ni
kaimu mhandisi,uendeshaji na matengenezo AUWSA,aliongeza kuwa changamoto kubwa
wanayoipata katika zoezi hilo ni pamoja na watu kujifungia ndani na kugoma
kutoa ushirikiano wakati wa zoezi hilo.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia