TAASISI YA KUKUZA SOKA ARUSHA YAJIVUNIA
TAASISI ya
kulea na kuendeleza vipaji vya soka nchini ya Future Stars Academy iliyopo jijini Arusha imejivunia kutoa wanasoka 6 kati
ya 23 waliochaguliwa kujiunga na kambi ya Manchester United jijini Nairobi
nchini Kenya mapema mwaka huu.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na mkurugenzi ambaye pia ni muasisi wa taasisi
hiyo,Alfred Itaeli alisema kwamba taasisi yao inajivunia kutoa wachezaji hao
ambao wawili ni wasichana na wanne ni
wavulana.
Aliwataja
wasichana waliochaguliwa kujiunga na kambi hiyo kuwa ni pamoja na Irene Baisi
na Jackline Gibson na kwa upande wa wanaume ni Suleman Yunus,Seleman
Msemo,Rasali Mustafa pamoja na Anthony Angelo.
Itaeli ,alisema
kwamba yeye kama muasisi ya taasisi hiyo anajisikia fahari kuwatoa wachezjai
hao kwa kuwa ni heshima kwa mkoa wa Arusha na nchi kwa ujumla.
“Ni fahari
kwa watoto na wana Arusha kwa ujumla wasichana hawa na kaka zao wamefanya kazi
kubwa na kujituma sasa wanaweza kuuona wakijiamnini na kusonga mbele”alisema
Itaeli
Hatahivyo,aliwapongeza
baadhi ya wadau ambao wamejituma kuhakikisha taasisi hiyo inasimama hadi sasa
hususani walimu wake,wazazi,watoto na wafadhili huku akisisitiza kwamba hiyo ni
hatua chanya katika dira sahihi.
Vijana hao ni
miongoni mwa vijana waliochaguliwa kuunda timu ya Tanzania kutoka michuano ya
Airtel Rising Satrs na watajiunga katika kambi ya Manchester United jijini
Nairobi huku wakitarajia kupambana na mataifa mengine 17 barani Afrika.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia