WATAKA KESI YA RUTO NA SANG KUANZA KUSIKILIZWA MACHI 2013
Mawakili wanaowatetea, Waziri wa Kenya, William Ruto
na mwandishi wa habari Joshua Sang Jumatatu waliiomba Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kuahirisha kuanza kusikilizwa kwa
kesi yao hadi baada ya uchaguzi wa Rais nchini Kenya, unaopangwa
kufanyika Machi 4, 2013.Upande wa mwendesha mashitaka haukupinga.
Mwendesha mashitaka, Florence
Darques-Lane alisema hapingi kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi ya
Wakenya hao katika kipindi cha miezi 10 ijayo lakini aliwaomba majaji
kutoa maamuziyao ‘’bila kujali tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi.’’
Aliwaomba pia majaji kuhakikisha
‘’bila kujali matokeo ya uchaguzi yatakuwaje, washitakiwa hao wahudhurie
mahakamani wakati wa usikilizwaji wa kesiyao.’’
Washitakiwa hao wawili wanakabiliwa
na mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu kwa kudaiwa kuhusika kwao
katika ghasia zilizotokea nchini mwao,baada ya uchaguzi wa rais Desemba
2007 ambapo watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kukosa mahali pa
kuishi.
Mwakilishi pekee wa waathirika wa
ghasia hizo, Sureta Chana, alipinga kuahirisha kwa shaurihilokwa muda
mrefu akidai kwamba wameshasubiri kwa zaidi ya miaka mitano kutendewa
haki.’’Waathirika wanataka kupata tarehe ya kuanza kusikilizwa kwa
shauri hili haraka iwezekanavyo,’’ aliiambia mahakama.’’
Nafikiri kuna
kiwango fulani cha kuishiwa uvumilivu kwa upande wa watu ambao bado
wanaendelea kuteseka kutokana na ghasia zilizotokea.’’
Awali kabla ya kusikiliza hoja
hizo,mawakili wa Ruto walielezea masikitoyaojuu ya kifo cha aliyekuwa
Waziri wa Usalama waKenya, George Saitoti baada ya kuanguka kwa
helikopta iliyombeba, Jumapili iliyopita na kuongeza kwamba alikuwa
shahidi mtarajiwa katika kesi hiyo.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia