SEKTA YA WAJASIRIA MALI WA KATI YATAKIWA KUKUZWA

MWENYEKITI  wa Chama  cha Kuweka na Kukopa cha Jumuiya ya Wazazi ya
Chama cha Mapinduzi (CCM )Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro (Siha
wazazi Saccos) Herman Mlale amesema kuwa ili  kuhakikisha uchumi wa
nchi unakuwa kwa kasi sekta ya wajasiriamali wa kati inatakiwa kukuzwa
kwa kupewa kipaumbele na kujengewa mazingira mazuri ya kibiashara.

Mlale aliya sema hayo  wakati wa kukabidhi hundi zenye thamani ya
shilingi milioni 6 .5 kwa wanachama wake sita ikiwa ni awamu ya kwanza
tangu kuanzishwa kwa Saccos na ni jambo la mafanikio kwa wanachama
wake  katika kupambana na umasikini.

Mlale  alisema fedha za kuwakopesha wanachama zilitokana na michango
yao hisa pamoja na riba wanazozipata kutokana na wanachama wao
wanavyoweka kila mwezi  za wanachama wa  ili waweze kupunguza
umasikini na kwamba lengo ni kujenga maisha yao  na  familia zao
pamoja na kuweza kuwapatia watoto wao elimu bora

Alisema mikopo wanayotoa inawekezwa katika sekta ya elimu, kilimo,
biashara ndogo ndogo na uvuvi na kwamba kutokana na ziada inayotokana
na shughuli ya ukopeshaji, Wazazi Saccos  pia inajihusisha na
kuwatembelea watoto wenye kuishi  katika mazingira magumu kwa
kuwapatia misaada .

Alisema ili kuongeza huduma za kifedha karibu na jamii kwa lengo la
kuwajengea tabia wananchi ya kujiwekea akiba, Saccos hiyo inaendesha
akaunti ya amana, ambayo inatoa huduma kwa wanachama na wasio
wanachama.

Akikabidhi hundi hizo Mkuu wa polisi wilayani Siha Lutusya Mwakyusa
aliwatka wanachama waliopatiwa fedha hizo kuhakikisha kuwa zinatumika
kwa malengo yalikusudiwa katika shughuli za ujasiriamali na si vingine
Mwakyusa alisema baadhi ya wanachama hutumia fedha za mikopo

wanazopatiwa na saccos kwa kubadilisha matumizi hali inayosababisha
kushindwa kurejesha marejesho kutokana na kutokufanya utafiti wa kile
wanachotakiwa kukifanya na fedha hiyo

Aliwataka wanachama wanaopatiwa mikopo kuwa wabunifu katika kufanya
shughuli za kijasiriamali na kuondokana na tabia za kuiga shughuli
zinazofanywa na mtu mwingine badala yake kila mmoja kufanya shughuli
kulingana na uwezo wake katika biashara .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post