MZEE RUKSA AZINDUA SAFARI YA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Mzee Mwinyi pamoja na Mkewe Mama Siti Mwinyi wakiongozana na mwenyeji wao mkuu wa wilaya ya Hai pamoja na kundi la Wapanda Mlima
wakipata maelezo
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga nae alikuwepo katika uzinduzi huo hapa akiwa anapanda mlima huo
Rais Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi asubuhi ameanzisha rasmi safari ya kupanda mlima kilimanjaro kwa mwaka huu inayoratibiwa kila mwaka na kampuni ya Geita Gold Mining LTD.
Kampeni hiyo ya mapambano dhidi ya Ukimwi na maambukizi ya Ukimwi  aliyoanza nayo Mzee Mwinyi tangu mwaka 2002 na inafahamika kama Kilimanjaro Climb against HIV/AIDS 2012
Mzee Mwinyi alifanya uzinduzi huo katika lango la Machame lililoko wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.
Kilichovutia zaidi ni kwa Mzee Ruksa kuwa fit kwa kipande alichotembea na leo kwa kiasi fulani alipunguza ule umbali anaopanda ambapo kila mwaka usababisha kati ya kundi lake la wapambe robo tatu kuishia njiani

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia