WATAKIWA KUACHA KUPUUZA SERA YA WAZEE
HALMASHAURI na Vituo
vya afya mbalimbali nchini zimetakiwa kuacha kupuuza sera ya wazee na badala
yake kuhakikisha kuwa wanafuta sera hiyo vema kwa kuwa baadhi ya wazee hapa
nchini wanakabiliwa na changamoto lukuki ikiwemo changamoto ya uhaba wa kipato
Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa na mwenyekiti wa chama cha
wazee (CHAWAMA) bw Eliniradhi Msuya wakati akiongea na wazee mbalimbali wa jiji
la Arusha mapema wiki hii.
Msuya alifafanua kuwa mtabia hiyo ya kuwakwepa wazee
inaendelea kuzaa matunda makubwa sana hapa
nchini kwa kuwa baadhi yao wanaonekana kama kero hasa katika vituo vya afya
Aliongeza kuwa wazee
kama wazee wanakabiliwa na changamoto lukuki hivyo ni jukumu la wahusika
kuhakikisha kuwa wanatekeleza sera mbalimbali za wazeee na wala sio kuwapuuza
kwa kuwa wana haki kwa mujibu wa sera yao
Pia alisema kuwa hata katika halmashauri nazo zinatakiwa
kuhakikisha kuwa zinakuwa na mafungu maalumu kwa ajili ya kuweza kuwasaidia
wazee ambao wengine ni walezi huku umri wao ukiwa umekwenda sana
Alieleza kuwa endapo kama wazee watatengewa bajeti yao
itakuwa ni raisi sana kuweza kubaini matatizo mbalimbali ambayo wanakabiliana
nayo hata kwa kupitia kwa chama hicho tofauti na sasa ambapo halmashauri nyingi
sana zinawakwepa wazee .
Awali mwenyekiti huyo aliwataka wadau wa elimu nao kuweza
kuwaangalia zaidi wazee hasa wale wa vijijini kwa kuwa baadhi yao wanakabiliwa
na changamoto ya kubwa sana ya kulea wajukuu huku wakiwa hawana kipato cha
uhakika,lakini kama wadau hao wakijitokeza kwa wingi na kisha kuwasaidia zoezi
hilo la kuwalea wajukuu basi watakuwa wamesaidia kwa kiwango cha hali ya juu
sana upatikanaji mzuri wa sera ya wazee hapa nchini.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia