KARIBU TENA TANZANIA
RAIS
wa Somalia Sheikh Sharif
Sheikh Ahmed akiagana na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete hivi leo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa kilimanjaro
RAIS
wa Somalia Sheikh Sharif
Sheikh Ahmed ameushukuru uongozi wa
serekali ya Tanzania kwa
jinsi wanavyoendelea kutoa misaada mbalimbali katika nchi yao.
Hayo
aliyasema jana (leo) wakati
alipokuwaakimaliza ziara yake ya siku tatu hapa nchini iliyokua na lengo la
kuomba misaada mbalimbali ya kibinadamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete na
serikali ya Tanzania.
Alisema
kuwa serekali ya Tanzania imekuwa
ikiwasaidia katika vitu mbalimbali hususa ni misaada ya kibinadamu kama vile vyakula kitu ambacho alimpongeza rais Jakaya
kikwete kwa kuwajali.
Rais
huyo ameondoka leo nchini akisindikizwa na Rais Kikwete asubuhi katika uwanja wa Kilimanjaro huku
ziara yake hiyo ikiwa ya mafanikio makubwa baada ya maombi yake kukubaliwa.
Kwa upande wa Rais Kikwete alisema serikali ya Tanzania itaendelea kutoka misaada mbalimbali ya
kibinadamu kwa serikali hiyo ya Somalia
kwakua tayari ilishaanza kutoa misaada hiyo hapo awali.
Aliongeza
kuwa tayari serikali yake ilishatoa misaada mbalimbali ikiwemo ya vyakula
ambapo jumla ya tani 500 za vyakula zilishatolewa ikijumuisha mahindi na ngano.
Aidha
Rais Kikwete alisema mbali na misaada hiyo ya vyakula pia serikali ya Tanzania ilishatoa misaada mingine ikiwemo
kuisemea Somalia
katika jumuiya mbalimbali juu ya matatizo ya machafuko yanayoikumba nchi hiyo.
Pia
alisema mbali na misaada hiyo pia Tanzania
itakua tayari kwaajili ya kuisaidia Somalia kwa kutoa wataalamu wake
mbalimbali kwenda nchini humo pamoja na kuwapokea wataalamu wan chi hiyo hapa
nchini ili kuwafundisha namna ya kuutengeneza na kuukuza uchumi wake.
“sisi
tulishaanza zamani kuisaidia Somalia
na nimeahidi kuendelea kuisaidia kwa misaada ya kibinadamu kama
vyakula matibabu pamoja na kutoa wataalamu wetu kwenda kufundisha namna ya
kuujenga upya uchumi wa nchi hiyo lakini sio masuala ya kiusalama kwa kutoa
majeshi yetu hapana”alisema Rais Kikwete.
Rais
Kikwete mara baada ya kumsindikiza Rais huyo alirejea mkoani Arusha tayari
kwaajili ya kuelekea mkoani Kilimanjaro leo jioni kwaajili ya shughuli ya
kilele cha maadhimisho ya sherehe za mazingira hapo kesho ambapo anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi.

0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia