Viongozi 2000 wa makanisa mbalimbali kutoka kati nchi 5 wanatarajia kukutana jijini Arusha na kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili nchi ya Tanzania ikiwa ni pamoja na mabadiliko ya tabia za nchi,pamoja na mapigano ya kidini yalioibuka zanzibar
Askofu wa makanisa ya Intenational Evangelism Centre ya hapa nchini Eliud Isangya alisema hayo wakati akifanya mahojiano na libeneke la kaskazini ofisini kwake ambapo alisema kuwa viongozi hao watakutana jijini hapa wiki ijayo
kwa sasa zipo changamoto kubwa sana ikiwemo changamoto ya mabadiliko ya tabia za nchi sasa kwa inawaasumbua wananchi wengi sana hasa wa vijijini lakini kama taasisi mbalimbali zikiwemo za dini zitawaamasisha hata waumini wake ni wazi kuwa jamii haitaweza kukumbwa na baa la ukame kwa maana hiyo tutajadili masuala kama hayo ambayo yanaitesa jamii za watanzania walio wengi
Aidha alibainisha kuwa wanasayansi wanabuni vitu vipya na vina uwezo wa kuwasaidia jamii kwanini sisi kama wadau wa nchi hii tusiwe wabunifu wa kusadia hata kuombea taifa katika majanga mbalimbali ambayo ni kikwazo cha maendeleo tunataka tufanye hivyo ili kurudisha hata vitu ambavyo vimepotea kwenye nchii hii ya Tanzania
Mbali na hayo Eliud alizitaka Taasisi nyingine za dini kuhakikisha kuwa kila mara zinayafanyia maombi changamoto ambazo zipo kwenye jamii kwa kuwa wao ndio wana nafasi kubwa sana ya kuweza kulikomboa taifa la Tanzania