Jeshi la wanamaji la Iran lapongezwa kwa kupambana na maharamia

Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibollah Sayyari amesema nchi nyingi duniani zimeshangazwa na mbinu za kipekee za jeshi la wanamaji wa Iran katika kupambana na maharamia.
Akizungumza wakati wa kuukaribisha Msafara wa 19 wa Meli za Jeshi la Wanamaji la Iran waliokuwa wakilinda doria katika maji ya kimataifa, Admeli Sayyari amesema; ‘jeshi la wanamaji la Iran limeyaonyesha madola ya kibeberu kuwa lina uwezo wa kudumisha usalama na amani katika eneo kwa kushirikiana na nchi za kieneo.' Admeli Sayyari ameongeza kuwa Jeshi la Wanamaji la Iran litaendeleza oparesheni zake maelfu ya kilomita kutoka pwani ya Iran kwa lengo la kulinda maslahi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Msafara wa 19 wa Meli za Jeshi la Wanamaji la Iran ulikuwa katika oparesheni ilioanza Machi 26 kaskazini mwa Bahari ya Hindi na Ghuba ya Aden.
Manoari za kivita za Iran zinalinda doria katika Ghuba ya Aden na Bahari ya Hindi kwa lengo la kukabiliana na maharamia. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya bahari IMO limepongeza mafanikio ya Jeshi la Wanamaji la Iran katika kupunguza uharamia.
 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post