wamama wakiwa wanasubiri usafiri wa kusafirisha mafuta ya taa yao yaliyokuwa yamefungashwa kwenye madumu
madumu yakiwa yamebeba mafuta ya taa ambayo wamepitisha katika njia za paya apo ni standi ya magari ya abiria holili
Serekali inakabiliwa na changamoto kubwa ya kudhibiti mapato yake kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wa holili mkoani kilamanjaro kwa kuwa biashara ya kuingiza mafuta ya taa hapa nchini kwa njia za panya imeshamiri kwa kasi kubwa kupitia mpaka huo.
Biashara hiyo na nyingine ya mahindi yanayovushwa kwenda Kenya kupitia njia za panya ambapo zipi zaidi ya 300 kwenye maeneo tofauti za wilaya nne mkoani hapo ikiwemo wilaya ya Same,Mwanga,Siha na Rombo imekuwa ngumu kwa vyombo vya dola kudhibitiwa au kukosa nyenzo za kukabiliana nazo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake meneja mkuu msaidizi wa mamlaka ya mapato mkoa wa kiliamanjaro Said Salum Hemed alisema kuwa ni kweli kumekuwa na wimbi kubwa la uvushwaji wa bidhaa ya mafuta ya taa hii inatokana na serekali kupandisha kodi kwenye bidhaa hiyo.
Alisema kuwa kwa sasa wamekuwa wanapata shida sana kwani kumekuwa na wafanyabiashara wengi ambao wanapitisha bidhaa hiyo ya mafuta ya taa bila kulipa kodi na wengi wao wamekuwa wakitumia njia za panya .
Alibainisha kuwa wao kama mamla ya mapato mkoani Kilimanjaro wamekuwa wanajitahidi kwa hali na mali kuthibiti upitishwaji huo wa mafuta ya taa lakini wanashindwa kutimiza lengo lao kwani kumekuwa na njia za panya nyingi ambazo wafanya biashara hao wamekuwa wanatumia kupitishia mafuta ya taa hayo.
“unajua kulingana na bei yetu ya mafuta ya taa kupanda sasa hawa wafanyabiashara wamejipatia dili kwani wamekuwa wanaenda huku kwa majirani zetu kuchukuwa mafuta ya taa na kupandisha hapa kwetu kwa ajili ya kufanya biashara sasa kibaya zaidi wana kwepa kulipa ushuru na kuamua kupitiasha katika izi njia za panya hali ambayo inasababisha hata pato la nchi halipatikanai vizuri “alisema hemed
Alisema kuwa watu wamekuwa wakikwepa uchakachuaji na hivyo bei ya bidhaa hiyo kupanda na kupelekea waagizaji wasio rasmi kuingiza nchini kwa njia za panya.
Aidha alibainisha kuwa biashara za mahindi na mafuta ya taa ndizo zilizoshamiri kwa sasa kwenye njia za panya na wao wanakabiliana nazo wakitumia kikosi chao cha fast na kuwaalaumu baadhi ya watendaji wasio waaminifu kukiuka maadili ya kazi zao hao ndio wanawapa changamoto kubwa katika utendaji wao wakazi za kila siku.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida waandishi waliweza kuona shehena za baadhi ya mazao yaliyokuwa kwenye baadhi ya viwambaza vya nyumba yakingojea kuvushwa kwenda nchi jirani ya Kenya na baadhi ya malori yaliyokuwa yanasubiri usiku uingie na kuvusha biashara zao najeshi la polisi limeendelea kulaumiwa na baadhi ya wananchi kwa kutokuwa na imani nalo kwa kudaiwa kuwa wanapokea kitu kidogo na kusindikiza baadhi ya magari kwenda upande wa pili.
Aidha waandishi wa habari walishuhudi baadhi ya pikipiki zikiwa na magaloni teyari kwenda kupakia bidha ya mafuta yataa na katika stnd ya mabasiwaliweza kuona magaloni yakiwa na mafuta ya taa na bidhaa mbali mbali .