BENKI ya Azania tawi la Mbauda jijini Arusha imewakabidhi zawadi mbalimbali baadhi ya washindi ambao ni wanafunzi walio katika mwaka wa kwanza katika vyuo vikuu vilivyopo mkoani Arusha zenye thamani ya sh,3 millioni baada ya wanafunzi hao kufungua akiba katika benki hiyo hivi karibuni.
Zawadi nyingine walizokabidhiwa wanafunzi hao wa vyuo ni pamoja na simu,ipod,flash disk ambapo mbali na kukabidhiwa zawadi hizo pia wamesisitizwa kujikita katika masomo kwa lengo la kulikomboa taifa katika umaskini pindi wamalizapo masomo yao.
Akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi mbalimbali zaidi ya wanafunzi 20 kutoka vyuo vikuu kadhaa vilivyopo mkoani hapa,meneja wa tawi hilo,Leonid Maliwa alisema kuwa benki yao imeanzisha utaratibu wa kutoa mikopo kwa wanafunzi hao kwa lengo la kuinua sekta ya elimu hapa nchini.
“Kwa sasa tumeanza utaratibu wa kutoa mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu hususani hawa wa mwaka wa kwanza lengo ni kuwaondolea kero lakini pia kuinua sekta ya elimu yetu hapa nchini”alisema Maliwa
Alisema kuwa mbali na kutoa mikopo hiyo pia benki yao pia inatoa huduma mbalimbali ya mikopo ya biashara,mikopo ya wafanyakazi pamoja na mikopo ya nyumba ambapo kwa sasa ni miongoni mwa benki nchini zilizoingia mkataba na shirika la nyumba la taifa(NHC) kutoa mikopo hiyo.
Hatahivyo,alibainisha ya kuwa mkakati wa benki yao kwa sasa ni kufungua matawi 4 katika mikoa ya Mwanza,Arusha,Dar es Salaam na Kilimanjaro ambapo kazi ya ufunguzi wa matawi hayo itafanywa kwa awamu mbalimbali.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia