WAPATIWA FURSA YA KUONGEZA WACHEZAJI


CHAMA cha soka wilayani Arusha(ADFA) kimetoa nafasi kwa timu zilizofanikiwa kutinga hatua  ya fainali kuongeza  idadi ya wachezaji watano katika usajili wa dirisha dogo lililoanza kufanyika jana novemba 19 hadi 24 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na katibu wa chama hicho,Zakayo Mjema alisema kuwa  kwa mujibu wa kanuni za ligi ya taifa inaipa mamlaka kamati tendaji ya chama chao kuongeza idadi hiyo lakini pia lengo ni kuzihimarisha timu zilizotinga fainali.

Alizitaja timu zilizotinga fainali ya kumpata bingwa wa wilaya kuwa ni Flamingo,Arusha Meat,Arusha Talent  pamoja na  Azimio ambapo zinataraji kumenyana katika fainali inayotaraji kuanza kutimua vumbi mnamo novemba 26 hadi  desemba10 mwaka huu.

Hatahivyo,alibainisha ya kuwa uongozi wa chama chao umeamua kuwafutia adhabu za kadi nyekundi na njano wachezaji wote wa timu zilizotinga hatua ya fainali  kwa lengo la kuwapa fursa wachezaji kucheza soka kwa kuwa kanuni zinaruhusu.

“Katika maamuzi mbalimbali tuliyofanya pia tumeamua kuwafutia kadi zote wachezaji waliokuwa wanazo kwa kuwa kanuni zinaturuhusu kuwapiga faini au kuwafutia lakini tunataka kuwapa fursa wacheze soka”alisema Mjema
 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post