AWATALA VIONGOZI WATOE ELIMU KWA WANANCHI WAO

Mkuu wa Wilaya ya Arusha Raymond Mushi amewataka Viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha kutoa elimu kwa wananchi kuhusu miradi mbalimbali inayoendelea katika maeneo yao ili waweze kujua manufaa ya mradi husika

Hatua hiyo ya Mkuu wa Wilaya imekuja baada ya kwenda jana kutembelea mradi wa barabara uliopo katika eneo la Lemara kati  mjini Arusha na kubaini kuwa Wananchi wa eneo hilo hawana elimu ya kutosha kuhusu mradi huo uliodhaminiwa na mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF)

Katika hatua hiyo bw.Mushi  alisema kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa Viongozi wetu kuwashirikisha wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo ikiwa nikuwapa elimu kwani kuna watu hawajui miradi inadhaminiwa na nani na nani hasa anafaidika na mradi huo

Kutokana na hali halisi iliyojitokeza katika ziara hiyo, imeonekana wazi kuwa ushirikishwaji juu ya mradi  wa barabara na familia ya Vavai haukufata taratibu kwani Mgogoro mkubwa uliibuka baina ya Halmashauri ya Manispaa ya  Arusha.

Mmoja wa familia ya Vavai Amos Vavai alisema kuwa wao hawapingi maendeleo ila katika mchakato huo hawakushirikishwa kwani waliporudi nyumbani walikuta nyumba zao zimewekwa alama ya X jambo ambalo kidogo iliwashtua sana

"Nimeshangaa sana kukuta alama ya X tena alama yenyewe ni rangi ya kijani na siyo nyekundu sasa kweli mtu anayetufanyia hivi ni diwani wetu Karim Moshi ambaye hakutaka kutushirikisha kwa hili je ni haki kweli au ni mambo ya siasa yanaendelea"alihoji Amos

Naye kaimu Mkurungezi wa Halmashauri ya Manispaa ya Arusha bw. Omary Mkombole alisema kuwa ushirikishwaji wa mchakato huo ulikuwa ni mdogo na ndicho hasa kilichopelekea watu kutoelewana

Aidha alisema haki itatendeka katika mchakato mzima ili kuweza kufikia malengo ya maendeleo katika jiji la Arusha kwani mbinu mbadala zitatumika kuleta uelewano baina ya wananchi ikiwa pia kuwapa elimu

Kwa upande wake Diwani wa Lemara kati Karim Moshi akijibu tuhuma hiyo alisema kuwa yeye kama diwani wa kata hiyo alikwenda kuwajulisha wananchi wake kuhusu mradi huo ila kutoelewa kulijitokeza hali iliyopelekea yeye kwenda kuweka alama za X wakiwa hawapo

"Nimewaelimisha juu ya hili ila wanaona kama ni mambo ya siasa ndo yanaendelea hapa na kuhusu mimi kutumia rangi ya kijani katika kuweka alama ya X ni kwamba niliishiwa na rangi"alisema Karim

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post