WALIMU ARUMERU WASHEREKEA SIKU YA MWALIMU NA MIAKA 50 YA CWT


picha ikionyesha walimu wa wilaya ya Arumeru  wakicheza katika sherehe za maathimisho ya siku ya mwalimu duniani na miaka 50 ya chama cha walimu Tanzania anaimba katikati ni mwalimu Saimoni ambaye alikuwa anaburudisha walimu wenzake mbele ya mgeni rasmi.

  Naibu waziri wa wizara ya   elimu na mafunzo ya ufundi Philipo Augustino Mulugo akiwa anakabithi kiti cha mwalimu ambaye ni mlemavu HAYUPO PICHANI ambacho atatumia kutembelea aendapo shuleni


walimu wakiwa katika maandamano kuelekea katika kiwanja cha  sos ambapo ndo walifanyia sherehe

 
SERIKALl imesema kuanzia mwakani ipo katika mchakato wa kuandaawaraka ambao utasambazwa kwa wakaguzi wa kanda,waratibu wa elimu katana kwa wakuu wa shule za msingi kote nchini,ambapo wanafunziwatakaochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza watatakiwa kuwa ni walewaliofaulu tu.

Naibu Waziri wa Elimu Mafunzo na ufundi Philip Mulugo aliyasema juzi wakati wa maadhimisho ya siku ya walimu duniani,yaliyofanyika
wilayani hapa mkoani Arusha.

Naibu huyo alisema kuwa atawawajibisha  wakuu wote wa shule za
msingi ambao watabainika kuwafaulisha wanafunzi na kuingia kidato cha kwanza bila kujua kusoma wala kuandika

Akizungumzia suala la shule ambazo hazijasajiliwa aliwataka waratibu wa elimu kata kuwajibika kwa madai kuwa shule nyingi zimekwua zikiendeshwa bila kusajiliwa kutokana na waratibu watendaji wa elimu kutowajibika kuanzia ngazi za chini.

Alisema kwua serikali  imepanga kutoa posho ya shilingi laki tano kwa waajiriwa wapya wanaporipoti katika vituo vipya vya vitakavyoainishwa kuwa viko katika mazingira magumu.

Naye Katibu wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT)mkoa wa
Arusha Nuru Shemkaro aliwataka walimu hao kuwa na mshikamano na chama chao ili kuweza  kutimiza majukumu na kutetea haki zao.

Aidha aliiomba serikali kutatua changamoto zinazowakabili walimu ikiwa ni pamoja kuongezewa kwa mishahara pale wanapopandishwa madaraja ili waweze kujikimu kimaisha kwani walimu wengi wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu kutokana na mishahara yao kwua midogo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post