BREAKING NEWS

Tuesday, November 1, 2011

WATAALAMU WA MASWALA YA JINSIA KUTOKA NCHI 11 ZA MAZIWA WAKUTANA ARUSHA

Wataalam wa masuala ya kijinsia kutoka nchi 11 za maziwa makuu wamekutana mjini Arusha, kujadili usawa wa kijinsia na ukatili wa kingono unaoendelea kushamiri barani Arfika kwenye siku za hivi karibuni , hasa kwenye mataifa yaliyoshamiri vita vya wenyewe kwa wenyewe ambayo ndio yameathirika zaidi.

Mkutano huo ulioanza leo jijini Arusha pamoja na mengine mengi utajadili maswala mbalimbali yanayozikabili Nchi za Maziwa makuu ikiwemo Tanzania ikiwa mojawapo ya nchi zinazokabiliwa na tatizo la jinsia licha ya kuwepo taarifa chache zinazoripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya sheria.

Pamoja na Nchi mbalimbali kusaini mikataba ya kisheria kupunguza ukatili wa kijinsia bado takwimu zinaendelea kuonyesha ongezeko kubwa kwenye ukatili wa kingono na jinsia barani Afrika husuasanai nchi zilizoathiliwa na vita 

 kama kongo (DRC) na Somalia
.

Akizungumza na waandishi wa habari mkurungezi wa maendeleo ya Jinsia kutoka Wizara ya maendeleo ya jamii Jinsia na watoto Meshack Ndaskoy, alisema ilikuepukana na hilo

Alisema kuwa wataalamu mbalimbali pamoja na Mashirika ya nje yatajadili kwa kina juu ya ukatili huo wa kingono na jinsia hivyo baada ya hapo muhtasari wake utapelekwa kwenye kikao cha Mawaziri wa nchi za maziwa makuu kitakachofanyika jijini hapa Novemba 4mwaka huu.

Aidha aliitaka Serikali pamoja na Mashirika mbalimbali kutumia zaidi utaratibu wa madawati na jamii iwe inatoa taarifa pindi inapokumbwa na majanga ya kubwakwa na kunyanyaswa kijinsia yanapotokea ili kuwepo na urahisi wa kushughulikia maswala kama hayo na jinsi ya kukabili nchi nyingi za Afrika ambazo bado vitendo hivyo vinashamiri kwa kasi na kufanya wimbi la ongezeko la ukatili wa kijinsia.
jamii inatakiwa kuelimishwa na kuwekewa mazingira mazuri zaidi ya uelewa juu ya ukatili wa kijinsia

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates