BREAKING NEWS

Thursday, October 27, 2011

KAIMU KAMANDA AKANUSHA KUMSAKA MFANYABIASHARA

JESHI la polisi mkoani Arusha limekanusha kumsaka Mfanyabiashara maarufu wa madini mkoani Arusha ,Dunstar Ng’unda (39)kwa madai ya kumtishia  kumuua mke wake wa ndoa,Jenipher Dunstar (35) kwa maneno , ikiwemo kumfukuza kwenye nyumba na kuipangisha.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha,Akili Mpwapwa alisema kuwa hana taarifa za kusakwa kwa mfanyabiashara huyo na kama zipo mlalamikaji anatakiwa awasilishe hati ya mashtaka aliyoifungua ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa .

Mpwapwa alisema kuwa taarifa za kusakwa kwa mfanyabiashara huyo amezisikia kupitia vyombo vya habari ila hakuwahi kupata tuhuma yoyote inayomhusu mfanyabaishara huyo,japo alikiri kupata taarifa za kutoelewana yeye na  mkewe

Hivi karibuni vyombo vya habari viliripoti taarifa za kusakwa kwa mfanyabiashara huyo,ambaye ilimlazimu kujisalimisha kwenye kituo cha polisi mjini Arusha,hata hivyo polisi ilipigwa na butwaa kwani haikuwa na taarifa yoyote inayomhusu na kumruhusu kuendelea na shughuli zake.

Akizungumzia suala la kutoelewana na mke wake wa ndoa,Ng’unda alisema hakuwa amegombana wala kumnyanyasa mkewe ,ila  nyumba waliokuwa wakiishi Plot namba 22,Block GG iliyopo eneo la Kimandolu mjini Arusha.

Waliamriwa kuondoka na mahakama , kufuatia kesi namba 53 ya mwaka 2010,iliyofunguliwa na baba yake mzazi baada ya kushindwa kumlipa kodi ya pango kwa muda mrefu,hatua ambayo mkewe aliipinga.

Kwa mujibu wa Ng’unda alisema kesi hiyo ilifunguliwa katika  mahakama ya Ardhi na Nyumba  mkoa wa Arusha ,ambapo iliendeshwa  na mwenyekiti wa baraza la Ardhi na Nyumba M. R. Makombe na kutoa  hukumu machi 23 mwaka huu,ikiwataka kuondoka mara moja katika nyumba hiyo. 

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo wanandoa hao waliendelea kuishi ndani ya nyumba hiyo na ndipo kampuni ya udalali ya majembe Auction Mart Ltd ilipopewa idhini  na mahakama, kuwaondoa kwa nguvu katika nyumba hiyo.

Ng’unda alisema kuwa mke wake hakuridhika na maamuzi ya mahakama hiyo na kuendelea kung’ang’ania kwenye nyumba hiyo hatua ambayo ilipelekea kuchukua maamuzi ya yeye kuhama na kuishi sehemu nyingine ili kuepusha ugomvi na baba yake mzazi ,mzee Isakwese Iduandumi Ng’unda .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates