Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Fulgence Kazaura (pichani) kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kipindi kingine cha miaka minne.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumanne, Oktoba 18, 2011, na Katibu Mkuu Kiongozi Phillemon Luhanjo imesema kuwa uteuzi huo unaanza mara moja leo hii.
Balozi Kazaura alikuwa Mkuu wa Chuo hicho katika kipindi kilichopita kilichoishia Julai, mwaka huu, 2011.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
18 Oktoba, 2011