BREAKING NEWS

Wednesday, October 5, 2011

AKUNAI AWATAKA WACHIMBAJI HARAMU WAONDOLEWE

Serikali imetakiwa kuwaondoa wachimbaji haramu wa
dhahabu katika mto yudhaya iliyopo wilayani mbulu ambapo uchimbaj
huo umesababisha kutokea kwa madhara makubwa katika eneo hilo
likiwemo la wanafunzi wa shule kutoroka mashuleni na kukimbilia huko
kufanya biashara za ngono.


Kauli hiyo na mbunge wa jimbo hilo Mustapha
Akunai wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na madhara yanayotokana na uchimbaji dhahabu
unaoendelea katika mto huo bila mpangilio maalumu na kuhatarisha
maisha ya wakazi wa eneo hilo.



Alisema mnamo mwa mwezi wa tatu dhahabu iligundulika katika mto huo na
kusamba katika maeneo mbali mbali mpaka kufikia m wilaya ya Karatu
hali iliyopelekea wavamiaji kutoka sehemu mbali mbali za nchi ambapo
wameweka makazi pembeni ya mto huo na hawana vyoo kwani maji hayo
yanategemewa na wananchi pamoja na mifugo.



Aidha alifafanua kuwa wachimbaji wapatao zaidi ya 600 wamesababisha
uharibifu wa mazingira na kisha kuweka mahema ambapo viongozi wote wa
kiserekali wana taarifa lakini inadaiwa hakuna jitihada zozote za
utekelazaji zilizochukuliwa dhidi yao hali


“mimi kama mbunge na wananchi wangu nimejaribu kufanya kila jitihada
za kuwaondoa wachimbaji hao imeshindikana lakini hii inatokana na
wachimbaji hao kutetewa na serikali ambao nina uhakika wanahisa zao
katika machimbo hayo maana wamelifumbia macho hili swala”Alisema
mbunge huyo

Aidha aieleza kuwa kutokana na wachimbaji hao kuchimba dhahabu bila
mpangilio wowte yametokea madhara kama vile magonjwa ya mlipuko
,wanafunzi wa shule za sekondar na msingi kutoroka na kukimbilia huko
huku wakifanya biashara haramu na za ngono hivyo kuipelekea wilaya
hiyo kurudi nyuma kimaendeleo.

Vile vile alidai kuwa endapo jeshi la wananchi linatumika kuzuia
sukari inayosafirishwa nchi za jirani serilaki inawezaje kushindwa
kuwazuia wavamizi hao kwani pamoja na hayo yote halmashauri hainufaiki
na chochote kutoka katika dhahabu hiyo hivyo ameiomba serikali
kuhakikisha inafuatilia hili swala haraka iwezekanavyo kabla wananchi
hawajaamua kufatilia wao wenyewe.



Alihitimisha kwa kueleza kuwa endapo hatua hiyo ya kuwaondoa
wavamizi hao watahakikisha kuwa wanamuweka muwekezaji wa kueleweka
katika mto huo ambaye atakuwa akifanya hiyo biashara kwani tangu mto
huo wa dhahabu kugundulika hawajawahi kunufaika na chochote kutoka
katika mto huo ambapo mapato yote yatakayopatikana yataingia katika
halimashauri..

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates