VIJANA UVCCM KUMSINDIKIZA MILLYA POLISI

VIJANA wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Wilayani Monduli pamoja na wa Mkoani Arusha jana waliandamana hadi Kituo Kikuu cha Polisi Mkoani hapa kumsindikiza Mwebyekiti wa Umoja wa Vijana (UVCCM) James Ole Millya ambaye alitakiwa kujisalimisha polisi na kudhibitisha kauli yake aliyoitoa kwenye mkutano wa Chama cha Mapinduzi wa kuzindua matawi.

Vijana hao waliandamana jana saa 5:00 asubuhi kuanzia Makao Makuu ya UVCCM hadi Makao Makuu ya Polisi huku wakiwa makundi wakisema wamekuja kumsindikiza Mwenyekiti Millya ili kujua kama atahojiwa au la .

"Tumekuja kumsindikiza mwenyekiti wetu kama polisi walivyomtaka aje na sisi tumekuja kumsindikiza ila hatujui atatokea wapi lakini anakuja maana mtu yupo hapa hapa Arusha lakini wanadai haatikani kwa simu na leo hii anakuja mwenyewe hizi ni siasa na hii ni vita basi kama vijana tuko nyuma yake kwa hili".

Baada ya kufika kituo cha Polisi vijana hao walikaa pembeni wakimsubiri Millya awasili na ilipotimu saa 12:00 Millya aliwasili kwakutumia gari lenye namba za usajili T457 AJV aina ya Landcruiser Lexus akiwa na wakili wake Mosses Mahunda na kusindikizwa na gari lingine namba T701 AGY lililokuwa na wazee .

Alipofika polisi vijana walikusanyika lakini waliambiwa na polisi waliokuwa maeneo hayo kutawanyika kwani eneo hilo ni dogo na vijana hao walitii amri hiyo na kwenda kumsubiri nje ndipo Millya na wakili Mahunda pamoja na baadhi ya viongozi wa UVCCM na wazee walikwenda ofisi ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Akili Mpwapwa ili kutii amri ya kutakiwa kujisalimisha lakini walipofika huko Mpwapwa aliomba afike leo kwani (jana) kulikuwa na shughuli za upokeaji wa mwenge na hivyo viongozi mbalimbali walikuwa huko.

"Naomba uje kesho asubuhi maana leo kunashughuli za Mwenge hivyo hatutaweza kufanya mahojiano"alisema Kaimu Kamanda Mpwapwa.

Baada ya kauli hiyo ,Millya pamoja na vijana wa Umoja huo walitoka wakitembea kwa miguu hadi ofisi za UVCCM Mkoa na kuongea na waandishi wa habari kuwa mpaka sasa hajui anaitwa kuhojiwa kwaajili gani lakini kesho ndio atajua anahojiwa kwasababu gani na hata alipofika polisi walimpokea na kumwambia kuwa aje kesho(leo) hivyo anasubiri ajue anaitiwa nini.

"Polisi ni sehemu salama na mtu yoyote anaweza kuitwa na kuhojiwa hivyo nasubiri nijue naitiwa nini mpaka sasa sijui naitwa kuhojiwa kwasababu gani hivyo wacha nisubiri nione ".

Wakati Millya akiongea nje ,Ofisi ya jengo la UVCCM ilikuwa imefungwa na kuwafanya vijana waliokusanyika hapo kuhoji ni kwanini Mwenyekiti huyo azungumze nje ya ofisi tena ikiwa imefungwa wakati ni ofisi yake na alitakiwa kuzungumzia mambo ya chama akiwa ndani ya ofisi na kuongeza kuwa hayo ni mapambano ili watayashinda.

Hivi karibuni Polisi Mkoani hapa ilimtaka Millya kufika Polisi kudhibitisha kauli yake aliyoitoa wiki iliyopita kwenye shughuli za ufunguaji matawi zilizofanywa na viongozi wa UVCCM ngazi ya Taifa na kutoa maneno kuwa kunamtoto wa kigogo ameshinikiza polisi kuzuia mkutano wao na polisi kusema kuwa watanhoji Millya kwa kauli zake ili awadhibitishie huyo mtoto wa kigogo aliyezuia mkutano huo ni nani na kama kunapolisi amezuia mkutano huo usifanyike ni nani.

Lakini Polisi walidai hawakuzuia mkutano huo bali Katibu wa UVCCM -Mkoa, Abdallah Mpokwa alilitaarifu jeshi la polisi kwa simu kuwa mkutano huo umeahirishwa lakini Oktoba 10 waliandamana bila kibali kwa kigezo cha kuwa wanafungua matawi ya wakereketwa kumbe wanafanya maandamano yasiyo na kibali huku wakitoa kauli za kutuhumu Polisi kuwa wanazuia mkutano wao na kigezo kuwa kunamtoto wa kigogo ametoa amri ya mkutano huo usifanyike.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post