BREAKING NEWS

Wednesday, October 26, 2011

KATIBU UVCCM AMTEMBELEA KIJANA ALIYEMWAGIWA TINDIKILA IGUNGA



katibu mkuu wa umoja wa vijana wa (UVCCM)Martine Shigela akiwa nazungumza na kijana Musa Tesha ambaye alimwagiwa tindikali Igunga


viongozi mbalimbali wa chama cha mapinduzi kutoka mkoani Arusha waliambatana na katibu wa UVCCM kwenda kumuangalia kijana huyo


kijana Musa Tesha (24) jinsi anavyoonekana akiwa amemwagiwa tindikali wakati wa  kampeni za uchaguzi Igunga kwa sasa yupo moshi kwa matibabu zaidi ila hali yake inaendelea vyema

Baadhi ya Vijana wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wa Mjini  Igunga waliohusika na kitendo cha kumwagia tindikali kijana mmoja ambaye ni mfuasi wa chama cha mapinduzi  wamelaaniwa vikali na katibu  mkuu wa Umoja wa vijana wa CCM(UVCCM) Taifa Martine Shigela kwa kufanya kitendo hicho cha kinyama na chakiuuwaji na kusema kuwa kufanya hivyo sio siosiasa bali ni upuuzi   .


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM(UVCCM) alilaani kitendo hicho mara baada ya kumuoana kija huyo ambaye kwa sasa yupo mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya matibabu ya jeraha hilo ambalo analo katika paji lake la uso pamoja na mkono na kusema kuwa waliousika na tukio hilo wamelaaniwa  hadi kwa mungu.


Katibu huyo aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati alipomtembelea Musa
Tesha(24) mkazi wa Igunga ambaye alikuwa anapatiwa Matibabu  katika hospitali ya
Rufaa ya KCMC baada ya kumwagiwa tindikali na wafuasi wa Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA),kwenye uzinduzi wa Kampeni za
uchaguzi huo.

“Kwakweli ni mehuzunishwa sana na vijana hawa waliohusika na kitendo hichi kwani kwani ni cha kiuhaji kabisa kweli unamwagia binadamu mwenzako tindikali unamuaribu kisa chama jamani mbona waliohusika na kitendo hichi wamekosa ubinadamu sasa kama wameanza kufanya siasa za hivi mapema hii huko tunapoenda sindio balaa"alisema Shigela

Alibainisha kuwa  ni jambo la kulaani kwa yeyote mpenda amani,inasikitisha pale
ambapo vijana wanatumika na vyama vya siasa kuharibu maisha ya wenzao.


Shigela aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanashirikiana katika mambo
ya msingi na kuwa na ushirikiano ili kuweza kujenga taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha James Ole Millya ambaye alikuwa ameongozana na Katibu huyo akizungumzia tukio hilo alisema kuwa kitendo hicho ni cha unayama na sio kizuri kwani watu wanakosa ubinadamu kwa sababu ya chama alisema kuwa Tanzania nchi ambayo inaamani aitakiwa kuwa ivyo kwani hata katika historia yake uko nyuma haiko ivyo.


"huu ni  unyama usiovumilika siasa zisitufikishe mahali ambapo mtu anaweza
kutoa roho ya mwenzake kwa sababu ya siasa,wanasiasa tunatakiwa
kushawishiana kwa hoja,hatuwezi tukagombania fito moja wakati sisi
wote  ni Watanzania na tunajenga nyumba moja”alisema  Millya

Akizungumzia  tukio hilo Musa ambaye ni Mkazi wa wilayani Igunga mkoani
Tabora,alisema kuwa siku ya tukio akiwa anabandika mabango ya Mgombea
wa kiti hicho cha ubunge kwa tiketi ya CCM,ghafla walitokea wafuasi wa
Chadema na kumkamata wakidai kuwa wanampeleka polisi.

Alidai kuwa siku ya tukio Sepemba 6 mwaka huu,vijana hao ambao
walikuwa ni wa Igunga Mjini,badala ya kumpeleka polisi kama
walivyokuwa wamemweleza,walimpeleka katika kichaka kidogo ambapo
walimvami na kummwagia tindikali usoni na katika mkono wake wa kulia.

"walinipeleka porini kisha wakanimwagia tindikali hii na kunipiga sasa baada ya kufanya vile nilijitaidi kujisogeza adi eneo la nyumba za watu nakwabahati nzuri  nikakuya nyumba moja karibu na pale nikagonga nao wakanisaidi awakatoa taarifa na nikasaidika kwakweli nawashukuru sana wale ambao wamenisaidia mpaka sasa na pia nashukuru sana chama kinavyonisaidia na pia nyie mliokuja kunitembelea nawashukuru wani jinsi mnavyokuaja mnazidi kunitia moyo"alisema Musa

Aidha baada ya kijana huyo kumwagiwa tindikali alipatiwa msaada na
wananchi waliokuwa karibu na eneo hilo,ambapo aliletwa mjini hapa kwa
ajili ya matibabu katika hospitali ya Rufaa ya KCMC,ambapo CCM
inagharamia gharama za matibabu yake.

Kwa sasa hali ya kijana huyo inaendelea vizuri ambapo juzi
aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo huku akiendelea kupatiwa matibabu
nyumbani kwa baba yake mdogo huku jicho la kulia likiwa halijafunguka huku lakushoto likiwa limefunguka na linaona kidogo japo kuwa bado linatiririsha machozi.


Naye Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Arusha kupitia umoja wa vijana (UVCCM) Catherini Magige alisema kuwa amesikitishwa sana na tukio hilo la kijana huyo aliyemwagiwa tindikali kwani ni cha kinyama na cha kiuhaji.

"unajua sisi ni watu wa baba mmoja kama ni mafundi tunajenga nyumba moja sasa kama tunajenga nyumba moja yanini kugombania fito za kujengea wakati nyumba ni moja tunajenga eeh jamani vijana wa kitanzania hatutakiwi kugombana hatutakiwi kutoana roho kwa ajili ya chama kimoja au kingine tunachotakiwa kufanya ni kukaa na kujadilia kuelimisha jinsi ya kujenga nchi yetu na sio kuvurugana"alisema Magige.

Kufuatia tukio hilo Katibu wa UVCCM taifa  aliahidi kiasi cha shilingi milioni 5
kutoka katika Jumuiya hiyo pamoja na kumpatia mtaji wa biashara kijana huyo pindi atakapo pona  na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Arusha kupitia(UVCCM) alimuahaidi kumpatia shilingi milioni moja za kumsogeza na kumsaidia pindi atakapo pona.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates