BREAKING NEWS

Sunday, October 9, 2011

DIAMOND MATATANI KWA UTAPELI ARUSHA - HAKUTOKEA KWENYE SHOW TRIPLE A

Vita ilipoanza pale walipogundua hamna msanii wameingizwa mjini

JESHI la polisi mkoni Arusha, linamsaka msanii nguli wa kizazi kipya wa jijini Dar es salaam,Nasibu Abdul Juma almaarufu Diamond kwa kosa la utapeli wa kujipatia kiasi cha shilingi milioni 1.5,na kushindwa kuhudhuria shoo jijini Arusha na kusababisha vurugu na uharibifu mkubwa wa mali katika ukumbi maarufu wa Triple A.

Diamond anadaiwa kuingia mkataba na kampuni ya Arbab mb Entertaiment ya jijini Tanga kuja kufanya shoo ya siku moja jijini hapa, siku ya ijumaa oktoba 8 mwaka huu ,baada ya kukubaliana kulipwa ujira wa shilingi milioni 2.5.

Hata hivyo msanii huyo aliingia mitini na kushindwa kuhudhuria shoo hiyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kutokana na kuachwa na ndege,hatua ambayo ilisababisha vurugu kubwa katika ukumbi huo ,kutoka kwa mashabiki waliokuwa wakitaka kurudishiwa kiingilio,ambapo katika vurugu hizo wacheza shoo wa msanii huyo na mwandaaji wa shoo hio walitiwa mbaroni na polisi .

Taarifa zaidi zimeeleza kwamba msanii huyo alilipwa kiasi cha shilingi milioni 1.5 sanjari na kukatiwa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi yenye thamani ya shilingi laki 3.5 ,ambapo aliwatanguliza wacheza shoo wake wanane jijini Arusha.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa kampuni iliyoanda shoo ya kumleta ,Diamond ya Arbab ,Mbwana Imamu alisema kuwa Diamond alishindwa kutokea na hakuwa ametoa taarifa yoyote ya kutofika kwake,kwenye shoo hiyo na kwamba muda wote walipokuwa wakiwasiliana kabla, alikuwa akimwambia anakuja.

Ilipofika usiku wa manane bila msanii huyo kutokea, mashabiki waliokuwa wametoa kiingilio ambao ni zaidi ya 2000 ,ndani ya ukumbi huo ,walianza kuleta fujo wakishinikiza kurudishiwa fedha za kiingilio kiasi cha shilingi 10,000 kila mmoja walizokuwa wamelipa.

Vurugu hizo ziliambatana na uvunjwaji wa viti,chupa,Glass,vioo ,thamani mbalimbali za ndani na watu kupigwa wakiwemo madj waliokuwa wakichezesha mziki.

Hata hivyo polisi waliarifiwa na kufika katika eneo hilo ambapo walimtia mbaroni ,mwandaaji wa shoo hiyo , Arbab pamoja na wacheza shoo wanne kati ya wanane wa diamond ambao bado wanashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mjini hapa,huku polisi ikimtaka msanii huyo kujisalimisha kituoni hapo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa The blue Triple A,Papa king alisema kuwa hasara iliyopatikana kutokana na vurugu hizo ni shilingi milioni 3.5 nakwamba imetia doa ukumbi huo unaoheshimika hapa nchini na Afrika mashariki.

Nae mkurugenzi wa Arbab ,Mbwana Imamu alisema kuwa msanii huyo amempatia hasara ya shilingi milioni 20 ambazo anamtaka kuzirudisha yakiwemo malipo ya uharibu wa ukumbi huo.

Diamond alipotafutwa kwa njia ya simu alisema kuwa hakufanya maksudi kutohudhuria shoo hiyo ,lakini aliachwa na ndege iliyokuwa iondoke majira ya saa 12 jioni katika uwanja wa ndege wa mwalimu Nyerere jana.

Hata hivyo alisema kuwa yupo tayari kufanya shoo yoyote bure katika ukumbi huo ili kufidia hasara hiyo iliyotokea.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Arusha ,Akili Mpwapwa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa bado wanawashikilia wacheza shoo wan ne wa Diamond kutokana na kosa la kusababisha vurugu n auharibifu uliotokea katika ukumbi huo wa Triple A na Diamond anatakiwa kujisalimisha katika kituo hicho cha polisi jijini Arusha.
wengine walikuwa wanendelea kupata kinywaji
Washabiki walio kuwa wanamsubiri msanii Diamond wakiserebuka wakati wanangoja aingie jukwaania

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates