BREAKING NEWS

Thursday, October 27, 2011

MAGESA MULONGO AAGIZA MTENDAJI NA MFANYA BIASHARA AWEKWE NDANI KWA WIZI WA SUKARI


Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiongea na wafanyabiashara wa sukari siku moja kabla ya kukutana nao 
askari wakiwa wamemuweka chini ya ulinzi mtendaji ambaye mkuu wa mkoa aliamuru apelekwe polisi kujibu alipopeleka sukari ya wananchi

Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amewaonya kwa vitendo baadhi ya wafanyabiashara pamoja na viongozi wa serikali ambao wamepewa dhamana ya kusimamia zoezi zima la ugawaji wa sukari, lakini wamekuwa wakihujumu zoezi hilo kwa kutowafikia wananchi hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaobanika.

Akizungumza katika mkutano wa wa watendaji wa kata,wenyeviti wa serikali za mitaa,madiwani  pamoja na wananchi wa kata ya Elerai katika manispaa ya jiji la Arusha kuhusiana na zoezi zima la ugawaji wa sukari ambapo katika kata hiyo wananchi walitoa malalamiko ya kutokuwa na imani na viongozi wa kijiji hali ambayo ilizua mvutano mkubwa baina ya viongozi wa vijiji ambao waliomba kusafishwa kama wananchi wanawatuhumu kuwa wanahujumu zoezi hilo.
Katika hali ya kushangaza mkuu wa mkoa Magesa alisema  wananchi hao walitoa malalamiko yao kuwa hawataki zoezi hilo lifanywe na viongozi wa vijiji,wenyeviti kwa kutokuwa na imani nao kwa madai ya kuchukua pese za wananchi na kutokomea nazo huku wakiongeza kuwa mtendaji wa kata alichukua sukari na kupeleka kata nyingine hali hiyo imewapelekea wananchi hao kukosa imani na viongozi hao.

Mbali na hayo siku moja  kabla ya mkutano huo kufanyika wananchi hao ambao ni wauzaji wa sukari waliandamana hadi kwa mkuu wa mkoa wakiwa wanataka sukari ambayo wanapata isigawiwe na watendaji wa kata kwani hawana imani nao hali ambayo ilimsabisha mkuu huyo wa mkoa kulazimika kuitisha mkutano wa wafanya biashara wa sukari na viongozi wao jana(leo).

Aidha mulongo alisema kuwa  kutokana na hali hyo ni lazima njia mbadala iumike ili wananchi wapate sukari kwa wakati na kwa bei elekezi ambapo amewataka wananchi wachaguane na kuteua mwenyekiti na zoezi zima walifanye wao na viongozi wa vijiji kazi yao kubwa ni kusimamia na kuhakikisha wananchi wanapata sukari.

Hata hivyo mulongo alihoji mbele ya wananchi mifuko 127 ya sukari  ambayo haijulikani ilipokwenda ambapo afisa mtendaji Joackim Kisarika alirusha tuhuma hizo kwa mfanyabiashara Salim Boyi ambapo aliitwa mbele ya mkuu wa mkoa na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na kurudisha shutuma hizo kwa afisa  mtendaji ambapo walikosa majibu hali iliyozua gumzo huenda kuna uchakahuaji ndani yake hivyo polisi walilazika kuwaweka chini ya ulinzi na kuwapeleka kituo cha polisi kwa kujibu ilipokwenda  mifuko 127 baada ya mkuu wa mkoa kutoa amri wakamatwe na wafikishwe mahakami kesho  na ikiwa watathibitika kuhusika hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Vile vile alisema  kuwa wafanya biashara wawataje kwa majina wanaohujumu zoezi hilo kwa makusudi kwani nia ya serikali ni kutafuta njia mbadala wa kuwasaidia wananchi kutokana na sukari kuuzwa kwa bei ya juu na kupelekwa mipakani kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi  hivyo wananchi kushindwa  kumudu gharama hizo.

Aliongeza kuwa  kuna wafanyabiashara wanachukua sukari na kutokomea nazo bila kuwafikia wananchi hali ambayo sukari hupotelea mikononi mwao hivyo amewataka wafuate taratibu na sukari ziwafukie wananchi tena kwa bei elekezi na atakaenda kinyume atachukuliwa hatua kali.

Pia aliwataka  viongozi kuacha siasa ambazo zimekuwa zikiingizwa hata kwenye mambo ya jamii bali watatue matatizo ya wananchi na watoe  huduma kwa wananchi kwa kufuata miiko ya kazi yao inavyosema kwa kuheshimina bila kujali elimu,wala itikadi za chama.

Aliwaasa vijana kufanya kazi kwa bidii na kushirikiana na serekali ili kuweza kupata maendeleo na sio kuleta fujo na kufanya maandamano yasiyokuwa na msingi kwa kushinikizwa na mtu yeyeyote.

"unajua nyinyi vijana wenzangu sasa ivi tunatakiwa tufanye kazi na sio  kusikiliza maneno ya watu wewe kweli na akili yako mtu anakuja kukushinikiza eti twendeni tuandamane adi kwa mkuu wa mkoa tukadai sukari wakati wewe mwenyewe unakazi zako na ulivyo unamfuata yule mtu unaandamana kudai sukari kwanini kwani si mnaviongozi wenu uliowachagua kwanini msiwatume acheni kufuata mkumbo bali fanyeni kitu kwa akili sasa ivi nataka tukae tufanye kazi tutengeneze mkoa wetu uwe na maendeleo na uendane na jina lake la jeniva ya afrika"alisema Magesa.

Aliwataka watendaji wa kata wasimamie sukari hiyo vizuri na waakikishe inauzwa kwa bei iliyopangwa na pia wailinde sukari hiyo iende kwa wananchi na sio kwa walanguzi ambao wanaenda kuchukuwa sukari na kuuza nchi jirani.
''nyie wenyeviti nataka mfatilie sukari hii vizuri mtu unayemuuzia muakikishe anapeleka dukani kwake kuuza kwa wananchi kwa bei iliyopangwa na sio yao kama imepagwa elfu na mia nane iuzwe iyo iyo ukikuta mtu anauza 2000 mchukulie sheria kwani anakiuka sheria "alisema

Alisema kuwa wao kama serekali wanatumia nguvu kubwa zaidi ili kuweza kuimarisha na kulinda sukari na wamemuonya vikali mtu wa mpkani na kumwambia atimize wajibu wake na aakikishe sukari haiendi nje ya nchi kupitia mipaka yake.

Aliongeza kuwa kwa sasa mkoa wa Arusha umekuwa ukitumia sukari nyingi zaidi kwani awali ilikuwa inatumia mifuko 1000 ya sukari kwa mwenzi lakini kwa sasa wanatumia mifuko 3000 kwa mwezi hali ambayo inawatia shaka kubwa na wanaanza kufatilia sababu .


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates