BREAKING NEWS

Wednesday, October 19, 2011

GARI LA MAHABUSU LAISHIA MAFUTA NJIANI MAHABUSU WAGEUKA MBOGO

GARI lililokuwa limebeba mahabusu "karandinga" leo limeshindwa
kuwafikisha mahabusu katika mahakama ya mwanzo ya Maji ya Chai iliyopo
wilayani Arumeru baada ya Karandinga hilo kuishiwa mafuta.

Adha hali hiyo ilijitokeza leo asubuhi kuanzia majira ya saa 3asubuhi katika
Mahakama Kuu Kanda ya Arusha wakati mahusubu waliokuwa na kesi katika
mahakama hiyo waliposhushwa na waliokwua na kesi katika mahakama ya
mwanzo walipokuwa wakisubiri kupelekwa huko.

Gari hilo lililokuwa na namba za usajili STG 9266 lilikwama kutoka
katika eneo la mahakama hiyo kutokana na kuishiwa mafuta.

Msajili wa mahakama hiyo Wilaya ya Arusha  George Herbert akizungumzia
tukio hilo alidai kuwa hana taarifa yoyote kuhusiana na tukio hilo .

"Mimi sijapata hizo taarifa ila nasikia kelele huko nje ila sijui ni
za nini,taarifa hizi ndiyo kwanza nazipata kutoka kwenu,kuhusiana na
hilo mtafuteni Kamanda wa polisi"alisema

Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Akili Mpwapwa alipoulizwa juu ya
tukio hilo alisema kuwa hadi hivi sasa hana taarifa za tukio hilo na
kudai kuwa taarifa za karandinga kuishiwa mafuta  ni la kawaida lakini
inapotokea hivyo dereva anatakiwa kutoa taarifa ili apewe mafuta na
kama atashindwa kufanya hivyo atakuwa mzembe.

"Mimi nashangaa sana kusikia taarifa hizo hadi sasa nianpoongea na
wewe sina taarifa hizo na asubuhi nilitoa lita 30 za mafuta wka ajili
ya gari la mahabusu na inawezekana wamefanya safari za ndani za
kupeleka mahabusu katika mahakama zilizopo hapa mjini na kuishiwa
mafuta lakini wakashindwa kutoa taarifa na hilo nasisitiza kuwa ni
uzembe"alisema

Mpwapwa alisema kuwa atafuatilia tukio hilo na kutoa taarifa sahihi.

Hata hivyo hadi libeneke hili linaondoka eneo la tukio majira ya saa 9
mchana mahabusu hao walikuwa bado ndani ya gari hili wakipiga kelele
za yowe,bila kujua hatma yao.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates