GARI YA HIFADHI YA MAMLAKA YA NGORONGORO LACHOMWA MOTO NA WANANCHI WENYE ASIRA KALI

GARI Lenye namba za usajili SU 34226 mali ya mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeteketezwa kwa moto na wananchi wenye hasira kali mara baada ya walinzi wa hifadhi hiyo kuwakamata wananchi.

Akiongelea tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha Akili Mpwapwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea october 16 majira ya saa moja na nusu jioni katika eneo kambi ya Simba kilichopo katika kitngoji cha Siaye kilichopo katika wilaya ya Karatu mkoani hapa.

Alisema kuwa wananchi wa eneo hilo waliokuwa na silaha za jadi walilivamia gari hilo na kulichoma moto mara baada ya wenzao kukamatwa na askari wa mamlaka hiyo ya hifadhi ya ngorongoro kutokana na kosa lakukutwa na mazao ya misitu aina ya Misandale.

"unajua mara baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa wanne waliokutwa na hii misandale ,waliitana wananchi wa eneo lile nakuanza kupiga mayowe ya kuitaana wakajikusanya wakiwa na silaha hizo kisha wakaenda kuleta fujo hizo na katika fujo hizo ndipo gari hiyo ya hifadhi ilichomwa moto"alisema Mpwapwa

Alisema kuwa askari ambao walikuwa na gari hili walijitaidi kuzima mapigano hayo kwa kupiga risasi hewani lakini hazikusaidia kwani wananchi wale waliendelea kuleta fujo na kuteketeza gari lote.

Alibainisha kuwa mpaka sasa kuna watu wanne wanashikiliwa kutokana na tuki hilo na bado upelelezi unaendelea wakuwasaka wote waliohusika na tukio hilo.

Aliwataja walioshikiliwa kuwa ni Stephano Gervas,Pascalina Raphael,Lidya Zakaria pamoja na Maria Ekonaay.

Alisema kuwa katika tukio hilo hakuna mathara yoyote yaliyotokea kwa binadamu.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post