BADO tasnia ya habari nchini imeelezwa kukumbwa na changamoto nyingi zikiwemo za kuruhusu matumizi ya lugha za vijiweni badala ya lugha fasaha hali ambayo ni miongoni mwa vyombo hivyo vya habari kuruhusu kuporomoka kwa tatizo la maadili licha kwamba kumekuwepo na tatizo la uandishi usiozingatia maadili kutoka kwa baadhi ya waandishi maarufu kama makanjanja.
Hayo yameelezwa na Mwezeshaji wa mafunzo ya maadili ya Uandishi wa habari Gervas Moshiro katika warsha ya siku mbili inayoendeshwa na Baraza la Habari nchini(BHT) kwa waandishi wa habari wa mikoa minne ya kanda ya kasikazini ya Tanga,Kilimanjaro,Arusha na Manyara yanayofanyika mjini Moshi inayolenga waandishi kuepuka kuacha kuumiza jamii.
Aidha alisema pamoja na kuwepo kwa jukumu la kuipasha habari lakini bado jukumu la kuipa jamii habari halijafikiwa ipasavyo kutokana na kutoridhiwa kwa kipengele kidogo cha Nne(d) cha ibara ya 18 cha katiba ya jamhuri ya Muungano ya Tanzania kinachosisitiza Haki ya kuwapa wananchi taarifa yakiwemo mambo muhimu kwa jamii ambacho hakijaridhiwa na serikali.
Akizungumzia changamoto hizo Moshiro amewataka waandishi wa habari hasa kuangalia habari zenye maslahi kwa jamii na sio kukandamiza na kuiumiza ili kutekeleza matakwa ya katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kifungu ibara ya 18 yanayosisitiza Haki ya jamii kupata habari lakini sio kwenda kinyume na maadili kama dhana kwamba vyombo hivyo vinakwenda na wakati .
Nae Mhandhiri toka chuo kikuu cha Tumaini Agnes Shija kwa upande mwingine amewataka waandishi kuanza kujikosoa,kujikumbusha kupeana ushirikiano ili kuleta mafanikio kwa jamii badala ya kwenda kinyume na maadili ya taaluma yao.
"niwajibu wa kila mwandishi kufuata maadili ya uwandishi wa habari na pia mwandishi kama mwandishi anatakiwa kujikosoa pamoja na kujitambua kabla ya kuandika habari yake na kuipeleka kwa uma"alisema Agnes
Alibainisha kuwa mwandishi wa habari anatakiwa kuthibitisha habari yake ni ya kweli kabla ya kuitoa anatakiwa awe ametumia haki katika uwandishi wake kama habari inamuhusu mtu anatakiwa aithibitishe kwa mlengwa na pia katika uwandishi wake atumie uadilifu na wakifuata hayo basi wataweza kusaidia uma na pia yeye mwenyewe ataweza kujiaminisha kwa wananchi.