RC ARUSHA AWAKUNA MADIWANI WA CHADEMA ASEMA WANAOKUJA KUFANYA MAPAMBANO ARUSHA ATAKULA NAO SAHANI MOJA,MADIWANI WACHUKIA, WAKIMBIA MKUTANO, WADAI KUWA NA WAO HAWAMTAMBUI RC NA MEYA



hapo madiwani wa Chadema wakiwa wanaondoka mara baada ya kutoka kwenye mkutano wa mkuu wa mmkoa
mmoja wa madiwani wa chadema akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutoka kwenye mkutano huo

Japo kuwa madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema walitoka katika mkutano huo lakini mkuu wa mkoa Magessa mulongo akutatarika na aliendelea na mkutano wake na watendaji pamoja na madiwani wengine waliobaki 

Ha li ya siasa kwa mkoa wa Arusha imeingia katiika sura nyingine mara baada ya mkuu wa mkoa wa arusha Bw Magesa Mulongo kusema kuwa  kamwe hatavumilia vitendo ambavyo vinaendelea katika jiji la arusha, ambapo ni pamoja na viongozi wa chadema kutaka kutawala mji huo wakati ndani ya majimbo yao hakuna vurugu, hali ambayo ilifanya baadhi ya madiwani na watendaji wa chadema kususa mkutano

Hayo yametokea jana wakati mkuu huyo wa mkoa akifanya mkutano na madiwani pamoja na watendaji mbalimbali  wa jiji la arusha ambapo mkutano huo ulilenga mikakati ya kuboresha zaidi jiji

Aidha Bw Mulongo alisema kuwa wapo baadhi ya wanasiasa ambao hawana nia njema na Arusha kwa kuwa kila mara wameonekana wakifanya vurugu huku ndani ya majimbo yao kukiwa shwari

Aliongeza kuwa hata maandamano ambayo yanafanywa na Chadema huku baadhi ya vijana wakiwa wanatoka katika mikoa na majimbo mengine hali ambayo inafanya machafuko makubwa huku ikiwa inawaumiza zaidi wananchi wa jiji hilo

“shangaa kwamba kiongozi wa kisiasa anakuja kupigana arusha kwake moshi au singida au karatu kupo shwari wanakuja na vijana wa kukodi kwa madai kuwa wana wanachama wengi sasa unamuweka wapi kijana au binti au mwananchi ambaye hajazoea vita nah ii ndio maana ya demokrasia kweli”aliuliza Bw Mulongo.
 
Katika hatua nyingine mkuu huyo alieleza hali ya vurugu ambayo inafanywa na wanasiasa huku wengine wakishinikiza zaidi maandamano hali ambayo nayo inazua sana tafrani kwa upande wa maendeleo ya mji wa arusha .

“ukishawaona wamekuja wanafanya vurugu alafu wanapelekwa mahakamani hapo hapo wanajitokeza watu ambao wanadai dhamana sasa inaonekana wanauwezo mkubwa sana wa kufanya vurugu na kasha kudai dhamana tujiulize wote wale mabinti zetu au vijana ambao hawana uwezo wa kupata dhamana na huku wakiwa ni wafuasi wao je wataishia wapi kama sio kuishia magereza na kwenye matatizo jamani“aliendelea kuhoji Mkuu huyo

Pia alisema kuwa kwa wale viongozi a,mbao kwa sasa ambao wanakesi mahakamani wanatakiwa kujua kuwa kwa kuwa mbele ya mkono wa sheria sio tija kwa jiji kukosa maendeleo kwa kuwa serikali bado ipo hai

Alisistiza kuwa kiongozi yoyote ambaye anajua kuwa ana kesi mahakamani anapswa kujitetea nafsi yake yeye mwenyewe na wala sio kuwashinikiza wananchi wamtete kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa wao ndio wasemaji wa mahakama  jambo ambalo mahaka ina taratibu zake.

“eti unakuta kiongozi amechaguliwa na wananchi ukiangalia sasa ni mwaka umekatika hamna ulichokifanya zaidi ya vurugu halafu unasema kuwa wananchi kuweni majasiri eti pamoja na ukombozi pamoja na ukamanda sasa basi kila kiongozi atawabeba mslaba wake baada ya muda mfupi na atawaeleza wananchi alichokifanya kumbukeni mimi siuzwi na wananchi ila nataka wananchi wajue uimu wa kiongozi bora ni upi”alisema
 
Bw Mulongo aliongeza kuwa kiongozi yoyote ambaye anajijua kuwa ana kesi mahakmani anatakiwa kujua na kutambua kuwa atabeba msalaba wake yeye mwenyewe na hapaswi kuwashirikisha wananchi kwa kuwa mlalamikaji au mlalamikiwa si msemaji wa mahakama.

Kutokana na kauli hizo za mkuu huyo zilisababisha madiwani wa chama cha chadema pamoja na watendaji wake kukimbia katika eneo hilo kwa kuwa walidai kuwa RC amewazalilisha sana

Wakiongea  mara baada ya kutoka katika eneo hilo walidai kuwa kama mkuu huyo angekuwa na shida ya kuwaona angesubiri mkutano uishe na wala sio kuwasema wao na chama choa katika mkutano

Waliongeza kuwa kutokana na hali hiyo kuanzia sasa hawataweza kumtambua mkuu huyo ambapo pia watahakikisha kuwa wanamktaa na kususa vikao au mahala popote alipo kwa kuwa yeye anaonekana kupendelea zaidi CCM

Walisema kuwa katika mkutano huo ulikuwa na lengo lakuzungumzia na kuboresha mambo mbalikmbali ya jiji la arusha na wala sio mahala  pa malukmbano baina ya CCM na CHADEMA.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post