ulinzi ulikuwa mkubwa wa hali ya juu kila kona kulikuwa na maaskari na silaha hali iliyowafanya wafuasi wa chadema wasije wengi
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa akiwa anashuka kwenye gari la mahabusu hivi leo
Mwanasheria wa Chadema ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Singida Tundu Lissu akiwa anashuka kwenye gari la mahabusu mara baada yakufika mahakamani
Wakiwa katika mahabusu ya mahakama wakisubiri kesi zao zitajwe
makamanda kizimbani
Mwenyekiti wa Chadema Dr.Slaa akisaini mara baada ya kupatiwa mthamana ili awe huru
Mbunge wa Singida Tundu Lissu akifurahia mara baada ya kupatiwa mthamana
Tundu Lissu na Dr.Slaa wakiwa wanajadili jambo na wakili wao Kimomogoro
wananchi walofika mahakamani wakimpokea mwenyekiti wao
Dr.Slaa akiongea na waandishi wa habari mara baada yakuotoka mahakamani
mkuu wamkoa wa Arusha Magesa Mulongo akiwa anafafanua jambo kwa waandishi wa habari waliofika ofisini kwake
waandishi waliwahi sana mahakamani kuwangoja viongozi hao wa Chadema na hapo walikuwa wanaendelea kubadilishana mawazo kuhusiana na sakata hili
Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa na mwanasheria wa chama hicho , Tundu Lissu na watu wengine 25 wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka matatu tofauti ikiwamo kufanya kusanyiko kinyume cha sheria , kukataa kutii amri halali ya polisi iliyowataka kutawanyika na la tatu ni la kutoa maneno ya uchochezi ambalo linamkabili Dk. Slaa .
Mashtaka hayo yalisomwa jana mbele ya hakimu , Devotha Kamuzora mwanasheria wa serikali , Haruna Matagane ambapo washitakiwa hao katika shauri hilo namba 451 la mwaka huu na washitakiwa wote wanatetewa na mawakili , Method Kimomogoro na Albert Msando .
Washitakiwa wote walikana shitaka ambapo 20 kati yao walidhaminiwa huku 7 wakikosa wadhamini na kupelekwa mahabusu ambapo wakili wao , Kimomogoro aliiomba mahakama endapo wakikamilisha taratibu za dhamana waweze kurejeshwa mahakamani hapo wasisubiri mpaka tarehe 22 novemba mwaka huu kesi yao itakapokuja kwa ajili ya kutajwa .
Katika shitaka la kwanza ilidaiwa mahakamani hapo kuwa washitakiwa wote kwa pamoja walikusanyika kwenye viwanja vya NMC kuanzia usiku wa novemba 7 , mwaka huu mpaka novemba 8, mwaka huu majira ya saa 12.00 asubuhi kwa lengo la kutenda kosa ambapo walikataa kutii amri halali ya polisi iliyoptolewa na Peter Mvulla ikiwataka kutawanyika .
Wakili Matagane alisema kuwa katika shitaka la pili washitakiwa hao siku ya tarehe 7 Novemba , mwaka huu majira ya usiku walikataa kutii amri halali ya polisi iliyotolewa na Peter Mvulla iliyowataka kutawanyika .
Katika shitaka la tatu linalomkabili Dk. Slaa peke yake alidaiwa kutoa maneno ya uchochezi mnamo Novemba 7 , mwaka huu majira ya saa 5.30 jioni kwenye viwanja vya NMC akimtaka IGP mwema amuamishe OCD Zuberi na kuwa watamng’oa Rais madarakani kwa maandamano .
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo alipoulizwa kama anahusika na kunyimwa kwa uzamini wa mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alisema kuwa yeye hausiki na kitu hicho swala hilo linashulikiwa na mahakama .
Alisema kuwa yeye anafanya kazi ambazo mkuu wa mkoa anatakiwa kufanya lakini sio kuingilia uhuru wa mahakama.
Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Slaa , Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu na wafuasi wao wamepandishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kutuhumiwa kufanya kusanyiko kinyume na sheria.
Mbali na mashitaka hayo Dk. Slaa pia anakabiliwa na shitaka lake peke yake la kudaiwa kutoa maneno ya uchochezi akiwa katika mkutano huo wa hadhara uliofanyika jana kwenye viwanja vya NMC.
Mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo Devotha Kamuzora,Mwendesha mashitaka wa serikali Haruni Matagane aliaambia Mahakama hiyo kwamba kosa la kwanza na la pili linawakabili watuhumiwa wote 27 ambalo ni kufanya kusanyiko kinyume cha sheria na kutokutii amri ya jeshi la polisi.
Akisoma shitaka la pili Haruna aliiambia mahakama hiyo Dk. Slaa anayekabiliwa na mashitaka ya uchochezi ambalo ni kosa la tatu anadaiwa kutoa kauli zenye uchochezi akidai kuwa atahamasisha wafuasi wake waaandamane hadi Magogoni Ikulu kuhakikisha wanamg;oa Rais Jakaya Kikwete.
Kipengele kingine kilichotajwa na mwendesha mashiataka huyo ni Dk. Slaa kutangaza kwamba watakodisha ndeghe kwa ajili ya kumbeba Mkuu wa Polisi wilaya ya Arusha Zuberi Mwobeji na kisha wampeleke Dar Es Salaam kwa IGP ili kumuuliza kwanini hadi leo hajamhamisha kazi OCD huyo.
Katika kesi hiyo upande wa watuhumniwa wote 27 unawakilishwa na mawakili wawili ambao ni Method Kimomogolo na Albert Msando ambao kwa pamoja waliiambia mahakama hiyo kuwa wateja wao walikuwa na watu wa kuwawekea dhamana kama mahakama hiyo itaona kuna umuhimu huo.
Kwa upande wake Hakimu Mkazi Devotha Kamuzura aliwaambiwa watuhumiwa kwamba dhamana yao ipo wazi lakini kwa masharti ya kila mtuhumiwa kuwa na wadhamini wawili na ahadi ya dhamana ya shilingi milioni tano.
Hata hivyo hadi mahakama hiyo inaashiriwa watuhumiwa 17 ndio walikuwa wamekiwisha kupata dhamana huku watuhumniwa tisa wadhamini wao wakishindwa kutimiza masharti ya dhamana.
Kesi hiyo itatajwa tena novemba22 mwaka huu mahakamani hapo.