BREAKING NEWS

Friday, November 11, 2011

TAMIDA YAITAKA SEREKALI KUPUNGUZA UTITIRI WA KODI

CHAMA  cha wanunuzi na wauzaji wa madini Tanzania (TAMIDA) kimeitaka serikali kuipunguzia mzigo wa utitiri wa kodi mbalimbli wanazotozwa na serikali kuu pamoja na halmashauri zake ambapo imelepelekea chama hicho kushindwa kujiendesha kuifanisi katika soko la ushindani wa kimataifa.

Akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa (TAMIDA) , uliowashirikisha wanunuzi na wauzaji wa madini  kutoka maeneo mbalimbali nchini, Mwenyekiti wa chama hicho , Sammy Mollel alisema kuwa, changamoto kubwa ni upatikanaji wa mikopo.

Alisema mabenki mengi nchini yamekuwana ukiritimba wa kutoa mkopo kwa wafanyabaishara wakubwa sanjari na kuweka masharti magumu, jambo ambalo limekuwa ni kikwazo kikubwa cha kufanikisha shughuli katika chama hicho.

Akitolea mfano tozo la VAT asilimia 18 katika biashara ya vito linawakwamisha katika kuendesha biashara ya vito hapa nchini  na kuwa kuchocheo cha kufanya baishara za magendo na kukidhiri kwa utoroshaji wa madini ya vito nje ya nchi na kusababisha hasara kubwa katika ukusanyaji mapato ya serikali.

Alisema ,sekta ya madini imekuwa ikikumbana na kodi mbalimbali ikiwa ni pamoja na dealer’s licence, VAT 18%,mirahaba (Royalties)kwa madini yote ghafi na yaliyosanifiwa,Payee, Payrol Levy 4%, Nssf 10%, Veta 2%,House Levy, Director’s Fee(kodi ya wakurugenzi), Application Fees for Export na SDL 6%.

Hata hivyo alisema kuwa, pamoja na changamoto hizo TAMIDA imeweza kufanikiwa kuboresha biashara ya madini kwa ajili ya kuongeza pato la taifa linalotokana na sekta hiyo pamoja na kuitangaza Tanzania kwenye minada mikubwa ya madini ya vito duniani.

Awali Kaimu Katibu Mkuu wizara ya nishati na madini,Eliakimu Maswi alisema kuwa,serikali itaendelea na mikakati yake katika kuimarisha sekta ya madini ya vito hususan sekta ya madini ya Tanzanite kwa kuanzisha hati ya uhalisia(Certificate of Origin)kwa madini yote yatakayosafirishwa nje ya nchi.

Alisema kuwa, serikali imeanzisha utaratibu wa kuahamasisha na kushawishi nchi ambazo zimekuwa zikinunua Tanzanite ghafi kwa wingi hasa India na Thailand kuja kuwekeza viwanda vya kusanifu madini hayo hapa nchini.

Aidha aliongeza kuwa, serikali imeanza kuzifanyia kazi changamoto zinazoikabili TAMIDA ikiwemo kuondolewa kwa VAT , kuanzishwa kwa benki kwa shughuli za madini , na leseni za shughuli za madini ikiwemo leseni ya usonara kutolewa na chombo  kimoja .

Maswi alisema kuwa, serikali kwa kushirikiana na TAMIDA imeandaa maonyesho ya kimataifa ya vito vya madini na usonara yatakayofanyika mjini Arusha mwaka 2012  na kuzishirikisha nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,Ethiopia, DRC, Msumbiji, Madagascar na Afrika Kusini.

‘Wafanyabishara na wachimbaji kuanzia sasa waandae madini mazuri ya kutosha ili wageni wakifika wasikose cha kununua katika maonyesho ya vito vya madini utakaofanyika mjini Arusha na hii ni fursa kubwa na ya pekee kwao kutangaza bidhaa zao kwani wageni''alisema

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates