Mwanasheria wa TLP akiwa anafafanua vifungu mbele ya waandishi wahabari
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi wa Arusha imetupilia mbali mashtaka na pingamizi lililofunguliwa mahakamani hapo na aliyekuwa diwani viti maalumu kupitia Chama cha TLP, Mwahija Choga dhidi ya uongozi wa chama hicho kuhusiana na kufukuzwa kwake uanachama pamoja na kutoa maamuzi ya kumvua uanachama na kusimamishwa udiwani.
Mahakama ilitupilia mbali mashtaka hayo , jana baada ya upande wa washtakiwa waliokuwa wakitetewa na Wakili Westgate Lumambo kujitosheleza katika maelezo yake na hivyo mahakama kuridhia kutupilia mbali.
Akisoma hukumu hiyo ,mahakamani hapo, Hakimu Mkazi wa Arusha,Anold Telekiano alisema kuwa, mlalamikaji ambaye aliwafungulia mashtaka uongozi huo mnamo June 23 ,2011 yenye namba 14/2011 pamoja na pingamizi namba 38 zote zikipinga yeye kufukuzwa uachama wa chama hicho kutoaka na kukiuka sheria za chama hicho.
Hata hivyo Hakimu huyo aliridhia maelezo yaliyotolewa na Wakili anayewatetea washtakiwa, yaliyokuwa yakiwema kuwa, mlalamikaji kisheria haruhusiwa kuwashatakiwa washatakiwa kwa vyeo vyao hivyo alivyofanya yeye nu kinyume cha sheria.
Ambapo katika kesi hiyo namba 38 aliyoiwakilisha mahakamani ilikuwa na pingamizi kuwa, uongozi wa chama hicho haurusiwi kumtangaza popote hadi mahakama itakapotoa hukumu yake , huku akiwakilisha barua ya kufukuzwa uanachama kuwa ni batili .
Hata hivyo katika mapingamizi hayo,yote mahakama ilitoa maamuzi ya kutupilia mbalimbali mashtaka hayo kutokana na kuwa hayakukithi na yalikuwa na mapungufu hivyo kumwamuru mshtakiwa huyo kusimamishwa uanachama ,pamoja na kuondolewa katika nafasi ya udiwani wa viti maalumu pamoja na ukatibu wa wilaya wa chama hicho.
Washtakiwa waliofunguliwa mashtaka mahakamani hapo, ni Leonard Makanzo-Mwenyekiti wa TLP mkoa, Mwamvua Wahanza –Katibu wa Tlp Mkoa, Mohamed Mahabadi –Katibu Mwenezi Mkoa, Jacob Molle- Mjumbe kamati ya utendaji mkoa, Salama Jumanne –Katibu wa wilaya Arusha, na Mjumbe wa kamati ya utendaji mkoa –Deodatus Humay , na Mwenyekiti wa Tlp Taifa , Augostino Mrema.
Hata hivyo,baada ya Diwani huyo kufukuzwa uanachama aliendelea kufanya shughuli za maendeleo na kuhudhuria vikao mbalimbali vya kichama ikiwemo baraza la madiwani pamoja na kuwa alikuwa tayari alishafukuzwa uachama na udiwani .
Ambapo baada ya uchaguzi kumalizika , wajumbe walifanya vikao na kumchagua Diwani Viti maalumu kuwa ni Mwamvua Wahanza lakini cha kushangaza jina la diwani Mwahija Choga likapitishwa na kuwa diwani pamoja na kuwa hakuchanguliwa na wajumbe .
Kutokana na hali hiyo ilizua mtafaruku mkubwa sana , huku wakihoji chanzo cha yeye kuwa diwani wakati aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo kisheria ni Mwamvua Wahanza , na kila alipokuwa akihojiwa alikuwa akijibu mkato , hali iliyopelekea kupelekena mahakamani ili kutafuta haki .
Baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, baadhi ya wanachama wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wa TLP mkoani hapa, Leonard Makanzo alisema kuwa amelipokea jambo hilo kwa furaha sana kwani lilikuwa likiwapa wakati mgumu sana , kwani wajumbe waliomchagua Mwamvua Wahanza walishangazwa sana na kitendo hicho cha kupewa udiwani Choga.
‘Kwa kweli nashukuru sana jambo hili limeisha salama na kisheria zaidi hivyop tunapenda umma na wanachama wetu wajue kuwa, diwani halali ni Mwamvua Wahanza na hatumtambui tena Choga kwani sio mwanachana wetu tena wala diwani na popote atakapokuwa akitumia chama chetu atachukuliwa hatua kali za kisheria’alisema Makanzo.
Diwani wa chama hicho kata ya Sokon 1, Marko Kivuyo alisema kuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Arusha, Estomih Changa’h anapaswa kutambua kuwa, Diwani aliyepitishwa rasmi na chama hicho nia Mwamvua Wahanza na sio Choga, hivyo haruhusiwi kuhudhuria vikao vyovyote katika halmashauri hiyo na watamwandikia barua ya kumtambulisha diwani huyo.