Ticker

6/recent/ticker-posts

TAMASHA LA UTAMADUNI WETU V/S BONGO FLAVA KUANZA KUANZA KESHO ARUSHA

 wasanii wa bongo flava madogo na domokaya wakiwa na kundi la mabaga freshi wakisikiliza semina
 mkufunzi akiwa anawapa somo wasanii wa ngoma ambao wanashiriki tamasha hilo
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa tamasha la kudumisha utamaduni wa muafrika linalotarajiwa kuanza rasmi kesho.

Akiongea na waandishi wa habari mratibu wa tamasha hilo Ismaili Mnikite alisema kuwa  tamasha hilo linashirikisha makabila mbalimbali yaliyopo ukanda wa kaskazini pamoja na wasanii wa muziki wa kizazi kipya (bongoflava) wa mikoa hii.

Alisema kuwa nia ya kuandaa tamasha hili ni kujaribu kuenzi utamaduni wa muafrika ikiwemo Ngoma za asili ,lugha,chakula pamoja na mila na desturi.

"pia katika tamasha hili tunatarajia kuangalia tofauti iliyopo katika ya muziki wa kizazi kipya yaani bongo flava pamoja na ngoma zetu za asili ambazo kwasasa zinakimbilia kupotea kutokana na miziki ya kigeni ambayo imetuingilia"alisema Mnikite.

Alibainisha kuwa pia watatumia tamasha hili kama sehemu ya kutanisha watu mbalimbali kutoka mikoa mbalimbali na makabila mbalimbali wakiwemo viongozi wa makabila mbalimbali ,viongozi wa dini pamoja na viongozi wa serekali.

Alitaja baadhi ya ngoma za makabila ambazo zitakuwepo ni wachaga,wamasai,wapare ,wambulu ,waberigeji pamoja man'gati .

Alisema kuwa sanjari na ngoma pia kila kabila litakuwa na chakula chake cha asili ambacho kabila hilo linatumia .

Aliwataja baadhi ya wasanii wa bongo flava ambao watakuwepo katika tamasha hilo kuwa ni pamoja na Fid Q,Afande sele,Nako 2 Nako ,Manidojo na domokaya pamoja na wengine wanaotoka mkoani hapa.

Aliwataja wathamini ambao wamethamini tamasha hili kuwa ni Ultimate,endelea foundation,claus fm,chanel ten,magic fm pamoja na KGS.

Alisewa tamasha hili ni endelevu  na alitoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Arusha wajitokeze kwa wingi kuangalia ngoma hizi za asili kwani hakuna kiiingilio  na alifafanua kuwa tamasha hili linafanyika katika viwanja vya general tyre vilivyopo njiro mkoani hapa.

pia tamasha hili liliambatana na semina ya siku moja ya utamaduni  ambao washiriki wate wa ngoma za asili pamoja na wasanii wa bongo flava ambayo mkufunzi alikuwa ni mratibu wa tamasha hilo

Post a Comment

0 Comments