Mkazi mmoja katika mji mdogo wa makambako Wilayani Njombe mkoani Iringa amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Njombe kwa tuhuma ya wizi wa simu ya mkononi.
Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu mfawidhi mkazi wa wilaya ya Njombe, Mwendesha mashtaka wa wilaya ya Bwana Andrew Mchome amesema mtuhumiwa GODFREY MWANGOKA aliiba simu ya bwana WANG WEL, yenye thamani ya shilingi laki tatu.
Mchome amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo april 26 mwaka huu.
Kwa upande wake hakimu mfawidhi mkazi wa mahakama hiyo FREDRICK LUKUNA amesema, upelelezi juu ya tukio hilo bado haujakamilika, na kesi hiyo itatajwa tena june 17 mwaka huu.