WAOMBA MSAADA WA MADAWATI NJOMBE

Wadau mbalimbali wa elimu wilayani njombe mkoani Iringa wameombwa kusaidia katika kutatua tatizo la uhaba wa madawati linaloikabili shule ya msingi igwachanya baada ya kukwama kwa malengo kuchonga madawati 100 kwenye harambee iliyofanyika hivi karibuni shuleni hapo.







Ombi hilo limetolewa na mwalimu mkuu wa shule hiyo bwana BETRANT MBENA,wakati akizungumza na uplands fm kuhusiana na mafanikio yaliyopatikana katika harambee hiyo ambapo shilingi laki tisa zimepatikana na kwamba pesa hizo zitatumika katika kuchonga madawati zaidi ya 60 tofauti na malengo yao ya madawati 100.







mwalimu mbena ameyataja matatizo mengine ambayo shule hiyo inakabiliwa nayo kuwa ni upungufu wa walimu ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi waliopo,uhaba wa mashine za kuchapa mitihani, maji ambapo amesema wanafunzi shuleni hapo hulazimika kuteka maji ya kunywa katika madimbwi,jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.







Akizungumzia hali hiyo afisa elimu wa shule za msingi wilayani hapa bwana kessy bartazar amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba wilaya ya njombe mpaka sasa imepokea walimu 90 ambao tayari wamekwisha kusambazwa mashuleni.







Bwana bartazar amesema serikali imeanzisha mkakati wa kudumu ikiwa ni pamoja na kufungua mfuko wa maendeleo ya elimu wilayani hapa ambao utasaidia katika ujenzi wa nyumba za walimu,kuwasomesha watoto yatima na kutatua matatizo mbalimbali yanayozikabili shule za msingi wilayani hapa.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post