BREAKING NEWS

Sunday, September 18, 2011

WAUDUMU WA AFYA 90 WAPATIWA MAFUNZO YA UGONJWA WA KISUKARI

Zaidi ya wahudumu wa Afya kwa jamii wapatao 90 kutoka wilaya tatu za mkoa wa Arusha wamenufaika na mafunzo ya ugonjwa wa kisukari na njia mballimbali za kukabiliana nazo katika jamii inayowazunguka.

Ambapo mafunzo hayo yamekuja baada ya kugundulika kuwa idadi kubwa ya jamii na wahudumu wa Afya hawana elimu ya kuweza kuwagundua wagonjwa hao kwa haraka hali inayopelekea kuwepo kwa ongezeko kubwa la wagonjwa hao na wakati mwingine kupelekea vifo vya mara kwa mara.

Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa na Chama cha ugonjwa wa kisukari Tanzania ,yanayofanyika mjini hapa yamewakutanisha washiriki hao kutoka wilaya ya Arumeru, Monduli na Arusha yanalenga kuwapatia elimu wahudumu hao ili waweze kufikisha ujumbe huo kwa wagonjwa waliopo katika maeneo yao kutokana na kuwa ugonjwa huo umekuwa ukienea kwa kasi kubwa sanabila kuchukuliwa tahadhari yoyote .

Meneja Mradi kutoka chama hicho, Ngoma Zakaria alisema kuwa, mafunzo hayo yanatolewa kupitia mradi wake wa 'Dear 'ambao ulianza mwaka 2009 na utamalizika 2012 na mradi huo upo katika nchi tatu za Kenya, Tanzania na Burundi huku programu hiyo ikifadhiliwa na European Commision pamoja na Hand Cup International .

Alisema kuwa, inalenga kufundisha wahudumu hao jinsi ya kutoa huduma katika maeneo yao kwa wagonjwa wa kisukari, kujua dalili zake, visababishi, na viashiria vyake pamoja na jinsi ya kuchukua matibabu kwa ujumla.

Alisema kuwa, lengo la kutoa mafunzo hayo ni baada ya kugundua kuwa kuna asilimia kubwa sana ya wagonjwa wa kisukari katika maeneo mbalimbali lakini wengi wao wamekuwa wakipoiteza maisha kutokana na kutokujua jinsi ya kuchukua tahadhari , hivyo kuwalazimu kutoa mafunzo hayo kwa wahudumu hao ili waweze kuielimisha jamii kwa ujumla.

Alisema kuwa, baada ya mafunzo hayo wataweza kukabiliana na ongezeko kubwa la wagonjwa wa kisukari linalojitokeza siku hadi siku kutokana na kuwa wengi wao wamekuwa wakiuchulia ugonjwa huo kuwa ni wa kishirikina na hivyo wengi wao kuishia kutumia tiba za asili ambazo hazisaidii chochote.

Alisema kuwa programu hiyo pia inalenga kutoa mafunzo kwa vikundi vya ili waweze kupelekea elimu hiyo ya ugonjwa wa kisukari kwa jamii inayowazunguka .

Naye Dr.Boniface Venance ambaye ni Mwezeshaji wa semina hiyo, alisema kuwa,changamoto kubwa iliyopo ni kutokana na ukosefu wa elimu kwa jamii na wahudumu juu ya ugonjwa huo , hivyo mafunzo hayo yatawawezesha kwa kiasi kikubwa kupunguza ugonjwa huo katika maeneo yao.

Alisema kuwa, asilimia kubwa ya jamii wamekuwa wakikimbilia kupata tiba kwa waganga wa kienyeji kutokana na mtazamo wao kuona kuwa ugonjwa huo unatokana na imani za kishirikina.

Venance alishauri elimu hiyo ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa mengine yasiyoambukiza yafundishwe katika vyuo vya Afya nchini ili kuwezesha kuwa na uelewa mapema kabla hawajaanza kuitumikia jamii .

Akizungumzia changamoto nyingine inayowakabili ni pamoja na upungufu wa bajeti kutoka serikalli kuu na wizara ya Afya na ustawi wa jamii na vitengo vyake ambayo inapelekea kutofikisha mafunzo hayo kwa wakati wa jamii nzima na hata wahudumu wa afya kupelekwa masomoni ndani na nje ya nchi mara kwa mara.

Aliitaka kuongezwa kwa bajeti ya wizara ya Afya ili iweze kushughulikia magonjwa sugu katikaupende wa elimu, kununua vifaa, tiba na madawa kwa ujumla kwani kwa kufanya hivyo ugonjwa huo utaweza kupungua kwa kiasi kikubwa sana .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates