picha PC Prosper akionyesha majeraha ambayo ameyapata baada ya kujeruliwa kwa risasi na majambazi
kaimu kamanda akionyesha silaha ambayo majambazi hao walikuwa wanatumi
kaimu kamanda wa polisiLeonard Paul akionyesha sehemu ambayo risasi ilipita ikampiga askari
gari la polisi likinyesha mawe ambayo yalikuwa yamewekwa barabarani na majambazi
WATU watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuwawa juzi na askari wa
jeshi la polisi mkoani hapa wakati walipokwua wakirushiana risasi na
askari hao.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kaimu Kamanda wa
Polisi Leonard Paul,alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 17
mwaka huu majira ya usiku katika eneo la Losiningoli Monduli.
Alisema jeshi hilo lilipata taarifa kutoka wka raia wema kuwa kuna
majambazi ambaow alikuwa wamepanga mawe barabarani kwa lengo la kuteka
magari yaliyokwua yamebeba abiria.
"Mara baada ya kupata taarifa hizo askari wetu walifuatilia hilo
tukio,walipofika katika eneo hilo majambazi hao walishtuka na kuanza
kurusha risasi kwa majibizano na katika varangati hilo askari wetu
walifanikiwa kuwapiga risasi majambazi watatu ambaow alifariki dunia
papo hapo"alisema
Kaimu huyo alisema kuwa majina ya majambazi waiwili hayakujikana na
ila walikuta kitambulisho cha mmoja wa majamabzi hao aliyemtaja kwa
jina la Joseph Marwa huku majmabazi wengine wawili wakitokomea
kusikojulikana.
Alisema kuwa katika tukio hilo walifanikiwa kukam,ata silaha aina ya
SMG ambayo majambazi hao walikuwa wanatumia hguku ikwia na risasi 25
ndani yake.
KATIKA tukio jingine Askari wa jeshi la polisi mwenye namba F 6004
PC Prosper amejeruhiwa vibaya na risasi katika mapaja mawili na
amajambazi wakati walipokuwa wanajibizana kwa risasi na majambazi hao.
Kaimu Kamanda alsiema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 2 usiku
katika eneo la Denish wilaya ya Arumeru barabara ya vumbi iendayo
Arumeru River Lodge.
Paul alisema kuwa katika tukio hilo askari hao waliokuwa katika gari
lenye namba za usajili T 709 AHY aina ya Nissan Terrano mali ya
Arumeru River Lodge ambapo askari hao walikuwa katika doria ya kawaida
kutokana na eneo hilo kuwa na tatizo la majambazi kupora watalii mara
kwa mara.
Alisema kuwa askari hao wakiwa katika doria ghafla lilitokea gari
lenye namba za usajili T 777 AGJ aina ya Toyota Land Cruiser mali ya
kampuni ya Unique Safari,likifuatiwa na gari aina ya Corola lililokuwa
na namba za usajili T 742 ANV ambalo lilikuwa limebeba majambazi hao.
Alisema kuwa agari hilo lililokuwa na askari ghafla liliona gogo kubwa
limewekwa barabarani ndipo wakaamua kupita pembeni ambapo majambazi
hao walianza kuwarushia risasi na gari dogo Corola ilipiwga risasi
katika matairi yote ya mbele na katika gari lilillokwua na askari hao
ambapo walipiga risasi ubavuni mwa gari hilo na kumjeruhi askari huyo.
Alisema kuwa katika majibizano hayo polisi walifanikiwa kumkamata
jambazi sugu mmoja huku wengine wakiwa wamekimbia.
Alisema kwua jina la jambazi huyo linahifadhiwa kwa sasa ili kuweza
kukamilsiah upelelezi na kudai kuwa jambazi huyo alikwua akitafutwa
kwa muda mrefu kwa kujihusisha na matukio mbalimbali ya uhalifu
likiwemo la mauaji Karatu pamoja na kukutwa na sialaha kinyume cha
sheria ambapo alisema jambazi huyo alitoka gerezani hivi karibuni.