BREAKING NEWS

Thursday, September 29, 2011

MFANYABIASHARA AWAWA NA WANANCHI WENYE ASIRA KALI

MFANYABIASHARA mmoja mkazi wa wilayani Arumeru mkoani Arusha
aliyetambulika wka jina la Lomayan Kisioki(37) amefariki dunia juzi
baada ya kupigwa na kisha kuchomwa moto na wananchibaada ya kudaiwa
kupora pikipiki

Mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa eneo
la Kwa Pole,lililopo kata ya Nduruama wilayani Arumeru mkoani
hapa,alifariki juzi majira ya saa sita mchana katika soko lililopo
eneo hilo.


Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Akili Mpwapwa alisema
kuwa wakati mfanyabiashara huyo akiendelea na shughuli zake ghafla
alivamiwa na kundi la watu.
ambao walipeleka marehemu huyo pembeni mwa barabara na kuanza kumpiga.

Alisema kuwa watu hao walimpiga mfanyabiashara huyo na
kumkatakata sehemu mbalimbali za mwili wake na kisha kumchoma moto.

Kamanda alisema kuwa watu hao walidai kuwa Kisioki
alikodisha pikipiki iliyokuwa na namba za usajili T 613 BNF iliyokuwa
ikiendeshwa na Frank Simon(30).

Alisema kuwa baada ya kukodisha pikipiki hiyo marehemu alimvamia
mwendesha pikipiki hiyo na kumpora,ambapo mmiliki wa pikipiki hiyo ni
Akundaeli Nanyaro.

Mpwapwa alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhi maiti katika hospitali ya mkoa ya Mt.Meru na uchunguzi juu
ya tukio hilo unaendelea.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates