BREAKING NEWS

Friday, September 30, 2011

MWANAFUNZI ATIWA MBORONI KWA KOSA LA KULAWITI

Mwanafunzi mmoja aliyejulikana kwa jina la Abdul Bitebo(17) Muha anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani hapa mara baada ya kutuhumiwa kumlawiti mwanafunzi mwenzake wa kidato cha pili.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Akili Mpwapwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea September 23 mwaka huu majira ya saa 8:15 usiku katika shule ya sekondari ya Edmund Rise iliyopo katika kata ya Sinoni ndani ya Halimashauri ya jiji la Arusha.

Alisema kuwa mwanafunzi huyo ambaye alimtaja kwa jina la Abdul Bitebo ambaye anasoma kidato cha nne katika shule Edmund alimlawiti mwanafunzi huyo wa kidato cha pili (jina linaifadhiwa) wakati wenzake walipokuwa wamelala.

Mpwapwa alibainisha kuwa mtuhumiwa alikuwa akipitia mabweni mbalimbali kuhakikisha kama wenzake wote wamelala na alipobaini wamelala alinyata taratibu hadi bwani lingine lijulikanalo kwa jina la Maisha Plus alipofika ndipo alifungua bwani hilo ambalo lilikuwa halijafungwa na funguo .

"sasa alipoingia kule bwenini alienda moja kwa moja hadi kwenye kile kitanda ambacho mwanafunzi huyo wa kidato cha pili ambaye ni mlalamikaji amelala ndipo akafunua blangeti na kumvua chupi na kuanza kumuingilia kinyume cha maumbile hali ambayo iliyomshtua mtuhumiwa kutoka usingizini "alisema Mpwapwa.

Alibainisha kuwa mtuhumiwa alikimbia mara baada ya kuona malamikaji ameshituka na akaacha baadhi ya vitu ambavyo alikuwa amevaa ambavyo ni ndala ila wakati akikimbia mlalamikaji aliweza kumtambua.

"sasa mara baada ya mtuhumiwa huyo kuamka lijiangalia ndipo alijikuta ametapakaa manii kwenye makalio yake hali ambayo ilimshutua na kumfanya atoe taaria katika uongozi wa juu wa shule ndipo uongozi wa juu wakaamua kufikisha taarifa za tukio hilo polisi"alisema Mpwapwa.

Aliongeza kuwa mara baada ya jeshi la polisi kupata taarifa hizo zilienda kumkamata mtuhumiwa na kufikisha polisi na walipomuhoji alikubali kuhusika na tukio hilo .

Kaimu kamanda alisema kuwa mpaka sasa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi zaidi unaendelea ili kubaini ukweli zaidi na utakapo kamilika atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates