MAMLAKA ya mawasiliano Tanzania(TCRA) imewataka watumiaji wa vifaa vya mawasiliano nchini, kutoa taarifa kwa mamlaka hiyo,pindi wanapobaini kwamba ,huduma wanayoipata haikidhi kiwango na ubora unaotakiwa.
Rai hiyo imetolewa na kaimu mkurugenzi na mratibu wa ofisi za kanda ,Victa Nkya katika semina ya wadau wa mawasiliano kanda ya kaskazini iliyofanyika wilayani Arumeru ,ikiwa na lengo la kuelimisha wadau na watumiaji wa vifaa vya mawasiliano.
Nkya alisema kuwa mara nyingi watumiaji wa mawasiliano wamekuwa hawajui haki na wajibu wao kuhusu mawasiliano,na pindi kunapotokea tatizo la mawasiliano ,hawajui mahala pa kukimbilia.
Hivyo kupitia semina hiyo aliwataka kutoa ushirikiano kwa mamlaka hiyo ili kama tatizo linatokana na watoa huduma waweze kufuatilia na kuwawajibisha wahusika ikiwemo kuwafungia, iwapo itabaini kuwepo kwa ukiukaji wa utoaji wa huduma hiyo.
Alisema kuwa pamoja na kupanuka kwa teknolojia ya mawasiliano nchini ,kumekuwepo na changamoto kubwa zinazotokana na utoaji huduma mbovu ,hususani kampuni za simu,Radio ,Intaneti, Luninga.
Alisema kuwa ni vema watumiaji wa vifaa vya mawasiliano wakatoa taarifa kwa TCRA ili hatua za haraka zichukuliwe kwakuwa mawasiliano ni muhimu sana duniani .
Alisema sera mpya ya mawasiliano duniani ni kuhakikisha kuwa ifikapo desemba mwaka 2015 vyombo vya mawasiliano hususani TV vinaingia kwenye teknolojia mpya ya digital na kuondokana na teknolojia ya Analogue ambayo imepitwa na wakati kwa kuwa imekuwa haina usikivu mzuri kwa vyombo vya mawasiliano.
Alisema kwa nchi za Afrika mashariki wamekuwabaliana kwamba ifikapo desemba mwaka 2012 ,wamiliki wote wa vituo vya luninga wawe wamehama kwenye Analogue na kujiunga kwenye digital.
Aidha aliwahimiza wamiliki wa vituo vya Luninga nchini kuanza mchakato wa kujisajiri kwenye kampuni tatu zilizopewa leseni na mamlaka hiyo, kutoa huduma ya digita,l ili pindi ifikapo muda huo ziwe zimejiunga kwenye kampuni hizo ambazo ni,Agape Associates,Star Times na Basic Transimission .
Kwa upande wa mgeni rasmi katika semina hiyo,katibu tawala wa halamashauri ya meru,Peter Mabuga aliitaka mamlaka hiyo kuhakikisha kwamba inasimamia vema huduma za mawasiliano zinazotolewa kwa makampuni mbalimbali yaliyopewa leseni ya kutoa huduma hiyo.
Aliitaka TCRA kutazama upya vipindi vinavyotolewa kwenye Luninga za hapa nchini,kwa kuwa vipindi hivyo ambavyo vinaonyeshwa kutoka za nje haviendani na mila na desturi za mtanzania.