MAJAMBAZI WAWILI WAKAMATWA WAKIWA NA SILAHA

Kaimu Kamanda wa polisi Arusha
Afande Akili Mpwapwa
Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa na bunduki katika nyumba wanaoyoishi.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa alisema kuwa tukio hilo lilitokea September 20 majira ya saa tatu na nusu asubuhi katika maeneo ya Sinoni katika kata ya daraja mbili mkoani hapa.
Alisema kuwa watu hao walikutwa na silaha aina ya Shotigan Papu Action-aina ya Moverickey Mossberg yenye no.MV 42155l Model 8812 GA ikiwa na risasi tano katika nyumba wanayoishi iliyopo katika eneo la Sinoni jijini hapa.

Aliwataja majambazi hao kuwa ni Salum Abudu (23)mchaga mkazi wa sinoni daraja mbili mungine ni Frank John alimaarufu kwa jina la Sankala (34) mkuria na nimkazi wa daraja mbili.

Alisema kuwa jeshi la polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema pamoja na wasiri wakati wakifuatilia watu waliohusika katika tukio lililotangazwa hivi karibuni la majambazi kumthuru askari .

Alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa hizo waliamua kufuatilia watu hao ndipo wakawakuta wakiwa na bunduki hiyo katika nyumba wanayoishi huku mmoja akikimbilia pasipo julikana .

“askari waliingia kupekuwa na kukuta silahi hii imefichwa pembeni ya kitanda ambapo ilikuwa imewekwa kwenye mfuko wa salfeti ikadumbukizwa kwenye begi alafu wakazungushia shuka juu”alisema Mpwapwa.

Alibainisha kuwa kwa uchunguzi wa awali walioufanya wamebaini kuwa majambazi hawa wameshajishuhulisha na moja ya tukio la mauaji ya silaha lililotokea katika kata ya daraja mbili

Alisema kuwa watuhumiwa hao bado wapo ndani kwa mahojiano na pindi upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashtaki likiwemo la kukutwa na silaha kinyume cha sheria.

"sasa katika hawa kuna mmoja ambaye ni watatu yeye alikimbia mapema hivyo bado jeshi la polisi linamsaka na pia tunaomba ushirikiano wa wananchi ili tuweze kumkamata"alisema Mpwapwa

Alisema kuwa anapenda kutoa wito kwa wananchi kwa ujumla kuwafichua watu ambao wanashauku nao pamoja na wanaowahisi ni majambazi ili waweze kuchukuliwa hatua mara moja kabla ya kufan ya mathara pamoja na uhalifu.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post