FA,MILIA ZA IDI YA 200 HATARINI KUBOMOLEWA NYUMBA ZAO ARUMERU

FAMILIA zaidi ya 200 wilayani Arumeru mkoani Arusha, zipo hatiani kukosa makazi ya kuishi na sehemu ya biashara,baada ya halmashauri ya Arusha kuziwekea alama ya X ikidai kwamba zimo ndani ya hifadhi ya barabara inayotarajiwa kupanuliwa yenye urefu wa kilometa tatu.


Wakizungumza na vyombo vya habari wananchi hao,wamesema kuwa halmashauri hiyo haikuwatendea haki kwakuwa tangu mchakato mzima wa kupanua barabara hiyo, itokayo Mianzini hadi Timbolo haikuwahi kuwashirikisha zaidi ya kuwawekea alama ya x ikiwataka wabomoe wenyewe nyumba hizo zinazoonekana kuwa ndani ya hifadhi ya barabara hiyo.


Wakitoa malalamiko yao,mmoja ya wananchi hao ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya waathirika,Fanueli Lamai alisema kuwa , wao hawazuii kupanuliwa kwa barabara hiyo ila kinachomsahanganza ni kutaka kujua anayewalipan fidia zao kwa nyumba zao zitakazovunjwa.

Alisema kuwa, pia wamekuwa hawashirikishwi katika mchakato huo wa upanuzi wa barabara na wala hawajui atakayewalipa fidia iwapo watapisha kwa hiari yao upanuzi wa barabara hiyo.


Aidha alisema kuwa, wanahitaji kuundwa kwa tume itakayoratibu utaratibu na kufuatailia mwenendo wa upanuzi wa barabara .


‘Unajua sisi tunapenda maendeleo sana kwa ajili yetu pia kwani barabara itakapopanuliwa ni mafanikio yetu pia ila kinachotupa wasiwasi ni nani atakayetulipa fidia zetu jamani na swala hili mbana hatushirikishwi tukiwa kama wananchi ambao ndio walengwa’alihoji .


Alifafanua zaidi kuwa, mwaka 2006 halmashauri hiyo iliwawekea alama ya X ambapo hawakupingana na kitendo hicho badala yake walitoa ushirikiano kwa kuvunja nyumba zao sehemu iliyozidi ,na kwamba alama hiyo tena imewekwa mapema mwezi huu ikisisitiza wavunje ambapo kwa mwaka huu alama hiyo imeingia ndani zaidi kuliko walivyotegemea

.

Aliongeza kuwa, hatua hiyo imepelekea kwa miongoni mwa wananchi kuingiwa na wasiwasi mkubwa kwani iwapo watavunja baadhi yao watakosa makazi kutokana na anyumba zao kumezwa na sehemu kubwa ya upanuzi wa barabara hiyo.


Alisema kuwa , athari hiyo ya bomoa bomoa itazikumba kata za Kiranyi, Olturoto , Moivo na Ilkiding’a ambapo wananchi hao walidai kuwa kuwa kuvunjwa kwa nyumba hizo kutawaadhiri wananchi walio wngi na kukosa makazi ya biashara kutokana na nyumba nyingi kujengwa karibu na hifadhi ya barabara hivyo kusababisha baadhi ya walio wengi kukosa makzi ya kuishi endapo hawatalipwa fidia.


Kwa upande wa mkurugenzi wa halmashuri ya Arusha, Khalifa Ida aliwataka wananchi hao kufuata utaratibu na sheria za kubomoa nyumba zote zilizozidi kwenye hifdhi ya barabara kwa kuwa mpango huo ni wa muda mrefu na kila mwananchi wa eneo hilo alifahamishwa.

‘Ninyi waandishi wa habari saidieni kuwaelimisha wananchi ambao wamewekewa alama ya X kutii sheria kwa kuwa nyumba zao zimejengwa ndani ya hifanyi ya barabara ili waweze kuzibomoa bila kushurutishwa .’alisema Ida.



Aidha alisema kuwa, mchakto wa upanuzi wa barabara hiyo utakapoanza watashirikishwa kupitia uongozi wao wa kijiji na kata .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post